• Nairobi
  • Last Updated March 5th, 2024 5:55 AM
Mamia ya watu waripotiwa kuuawa katika vita magharibi mwa Sudan

Mamia ya watu waripotiwa kuuawa katika vita magharibi mwa Sudan

Na XINHUA

KHARTOUM, SUDAN

MAMIA ya watu wameuawa na wengine kudhulumiwa katika mapigano katika jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan, kulingana na ripoti zilitolewa na mashirika ya nchi hiyo na yale ya kimataifa.

Shirika la Kimataifa kuhusu Uhamiaji (IOM) lilisema kwenye taarifa kwamba karibu watu 700 wameripotiwa kuuawa, 100 kujeruhiwa na wengine 300 haijulikani waliko katika jimbo hilo kufuatia mapigano kati ya wanajeshi wa Sudan (SAF) na wapiganaji wa kundi la Rapid Support Forces (RSF) katika eneo la El Geneina.

Nalo Shirika la Kutetea Haki za Kibinadamu la Al-Juzoor linasema watu 1,300 waliuawa na wengine zaidi ya 2,000 wakajeruhiwa katika eneo la Ardamata.

Kwa upande mwingine, kundi la kutetea haki ya umma ya West Darfur State Revolutionaries Bloc lilisema kuwa watu 2,000 waliuawa na wengine 3,000 wamejeruhiwa katika vita hivyo vilivyodumu kati ya Jumatatu na Ijumaa wiki hii.

Awali, mnamo Alhamisi Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Kutoa Usaidizi Sudan (UNITAMS) kilisema kuwa kundi la RSF kutwaa udhibiti wa kambi ya SAF, wapiganaji wanaounga mkono RSF walitekeleza vitendo vya ukiukaji haki katika kitongoji cha Ardamata, eneo la El Geneina.

Ripoti zinasema kuwa wapiganaji wa Kiarabu waliuawa raia kadha na kuwajeruhi watu wengine wengi katika jamii ya Masalit.

UNITAMS ilielezea hofu kuwa vita hivyo vinasababisha athari kubwa kwa raia na kutoa wito kwa pande hasimu kuzingatia wajibu wao wa kulinda maisha ya raia wakati wa makabiliano hayo.

Aidha, ubalozi wa Amerika jijini Khartoum ulitoa taarifa ukielezea hofu yake kuhusu vitendo vya ukiukaji wa haki za kibinadamu vinavyotekelezwa na kundi la RSF na wapiganaji wanaoliunga mkono.

  • Tags

You can share this post!

Mashindano ya kuogelea ya kaunti ya Kiambu yapigwa jeki na...

Simbas, Lionesses kwenye mizani ya timu za Uganda katika...

T L