• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 9:50 AM
Mbunge wa Uingereza ajiuzulu kwa kosa la kutazama video chafu bungeni

Mbunge wa Uingereza ajiuzulu kwa kosa la kutazama video chafu bungeni

NA MASHIRIKA

LONDON, Uingereza

MBUNGE mmoja wa chama cha Conservative chake Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, Jumamosi, Aprili 30, 2022, alijiuzulu baada ya kupatikana akitizama video chafu za ngono akiwa bungeni.

Ilisemekana kuwa Neil Parish alitizama video hiyo ya ngono kutoka kwa simu yake ya mkono mara mbili akiwa bungeni.

Mbunge huyo mwenye umri wa miaka 65 aliwaambia wanahabari kwamba mara ya kwanza alipotazama video hizo ilikuwa ni kwa bahati mbaya kwa sababu alikuwa akisaka magari mitandaoni.

“Mara ya pili ilikuwa ni kimakusudi na kama kitendo kilichosababishwa na hali ya wenda wazimu,” akawaambia wanahabari Jumamosi alipokuwa akitangaza kujiuzulu kwake.

Muungano wa wabunge wa Conservative magharibi mwa Uingereza uliunga mkono kujiuzulu kwa Parish.

“Tungependa kuchukua fursa hii kumshukuru Neil Parish kwa huduma yake kwa jamii yetu kwa miaka 12 iliyopita. Tunaunga mkono uamuzi wake wa kujiuzulu kama Mbunge wetu,” muungano huo ukasema kwenye taarifa kutoka Tiverton and Honiton.

Serikali ya Waziri Mkuu Johnson wakati huu inazongwa na kashfa nyingi, siku chache kabla ya chaguzi za baraza ya miji kuandaliwa.

Bw Johnson mwenyewe amepigwa faini na polisi kwa kukiuka kanuni za kuzuia kuenea kwa Covid-19 mnamo 2020.

Tafsiri Na: CHARLES WASONGA

  • Tags

You can share this post!

Wapwani washauriwa wakome kubagua wanaougua Ukimwi

Joho aapa kuzima Sonko Mombasa

T L