• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 9:55 AM
Mfalme Charles III atawazwa rasmi kwenye sherehe babukubwa

Mfalme Charles III atawazwa rasmi kwenye sherehe babukubwa

NA MASHIRIKA

LONDON, UINGEREZA

MFALME Charles III amekula kiapo kwenye sherehe ya kipekee iliyoandaliwa Jumamosi, Mei 06, 2023 akiahidi kuwa mtumishi wa Muungano wa Britania unaojumuisha Uingereza, Wales na Scotland, pamoja na Ireland ya Kaskazini.

Mfalme Charles III na mkewe Camilla wamesafiri kwenye Gari Maalum kwenye Msafara wa Mfalme kwa umbali wa kilomita mbili kutoka kwa Kasri la Buckingham hadi Westminster Abbey katikati mwa jiji la London.

Mfalme Charles III na mkewe Camilla wamesafiri kwenye Gari Maalum kwenye ‘Msafara wa Mfalme’ kwa umbali wa kilomita mbili kutoka kwa Kasri la Buckingham hadi Westminster Abbey katikati mwa jiji la London mnamo Mei 6, 2023 kutawazwa rasmi. PICHA | AFP

Hafla hii spesheli ni ya kwanza kwa Uingereza kwa kipindi cha miaka 70.

Aidha, ndiyo ya pili katika historia kupeperushwa kwa runinga.

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amehudhuria sherehe hiyo ambapo amesoma maandiko kutoka kwa Agano Jipya.

Rais wa Kenya Dkt William Ruto ni miongoni mwa wageni walioalikwa kwenye sherehe hiyo.

Charles III, ambaye amevikwa taji kichwani saa sita na dakika mbili adhuhuri saa za London na Askofu wa Canterbury Justin Welby, ndiye wa 40 tangu kutawazwa kwa Mfalme William I mwaka 1066.

Alirithi ufalme mnamo Septemba 8, 2022 kufuatia kifo cha mamake Elizabeth II ambaye alikuwa Malkia tangu Februari 6, 1952 alipomrithi Mfalme George VI. Wakati huo Charles alikuwa na umri wa miaka mitatu pekee.

Nje ya Muungano wa Britania, Charles III anakuwa pia mfalme wa mataifa mengine 14 ya Jumuiya ya Madola – Commonwealth – ambayo yanajumuisha Australia, Canada na New Zealand.

Camilla, ambaye ni mke wake wa pili, naye ametawazwa kuwa Malkia Camilla dakika 15 baada ya sherehe kuu.

Baadaye Msafara wa Mfalme umefululiza hadi kwa Kasri la Buckingham ambapo Gari Maalum linalobururwa na farasi limeingia saa saba na dakika 35 sawa na saa tisa na dakika 35 saa za Afrika Mashariki.

  • Tags

You can share this post!

NYOTA WA WIKI: Callum Wilson

Mashabiki wa AFC Leopards waruhusiwa kurejea uwanjani

T L