• Nairobi
  • Last Updated May 13th, 2024 2:11 PM
Papa Francis aongoza Jumapili ya Mitende

Papa Francis aongoza Jumapili ya Mitende

PAPA Francis leo Jumapili amewaongoza maelfu ya waumini wa Kanisa Katoliki kusherehekea Jumapili ya Mitende siku moja baada ya kuruhusiwa kuondoka hospitalini.

Kiongozi huyo alikuwa amelazwa kutokana matatizo ya kupumua.

Kwenye ujumbe wake, ameirai dunia kuwajali watu maskini, wapweke na wenye akili punguani.

Maelfu ya watu waliinua mitende na matawi ya mizeituni wakati alipowasili katika Kanisa la St Peter’s Square Basilica, jijini Vatican, akiwa nyuma na kijigari maalum cheupe.

Baadaye, alishuka na kuanza kuongoza misa akiwa nyuma ya chumba kimoja kikongwe.

Papa Francis, 86, alilazwa katika Hospitali ya Gemelli, jijini Roma, Italia, Jumatano iliyopita, baada ya kulalamikia matatizo ya kupumua.

Hata hivyo, alipata nafuu haraka baaada ya kupewa dawa za kukabiliana maumivu aliyokuwa nayo.

Baadaye, alirejea katika makazi yake ya Vatican, Jumamosi.

Katika juhudi za kuondoa wasiwasi wowote kuhusu hali yake ya afya, Vatican imesema kuwa kiongozi huyo atashiriki katika shughuli zote zinazohusu maadhimisho ya Sikukuu ya Pasaka wiki hii.

Msimu huu ndio huwa wenye shughuli nyingi zaidi katika kalenda ya Kanisa Katoliki.

Akiwa amevalia mavazi mekundu, Papa aliziungumza kwa sauti tulivu, japo iliyosikika vizuri, alipouhutubia umati wa zaidi ya washiriki 30,000 waliofika. Aliwarai washiriki hao kutowapuuza au kuwasahau wale wanaokumbwa na matatizo.

“Leo, idadi yao ni kubwa sana. Watu hao wameachwa, kutelekezwa huku wengine wakihangaika. Maskini huwa wanaishi katika barabara tunazopitia ila huwa tunawapuuza. Idadi ya wahamiaji pia inaendelea kuongezeka, hakuna anayetaka kuwashughulikia wafungwa, watu huwa wanawapuuza,” akasema.

Hafla hiyo ndiyo ilikuwa ya kumi inayohusu maadhimisho ya Pasaka kuiongoza tangu kuchukua uongozi wa kanisa hilo mnamo 2013.

Katika hotuba yake yote, alitilia mkazo matatizo yanayowakumba watu maskini na wahamiaji.Katika miaka ya hivi karibuni, kiongozi huyo amekuwa akikumbwa na matatizo kadhaa ya kiafya, moja ikiwa tatizo la goti. Ni hali ambayo imemfanya kuanza kutembea kwa kutumia kijiti au kijigari maalum katika maeneo ya umma.

Ugumu ambao amekuwa akikabiliana nao kutembea umemfanya kutoshiriki katika baadhi ya hafla muhimu, kama mwaka 2022.

Jumapili ya Mitende huwa inaashiria wakati Yesu aliwasili jijini Yerusalemu kwa kutumia punda, huku akishangiliwa na umati mkubwa wa wafuasi wake. Wakristo huwa wanaamini alifufuka kutoka kwa wafu baada ya kusulubiwa Msalabani.

Katika Alhamisi Takatifu, Papa Francis ataongoza misa maalum kwa watoto walio gerezani jijini Roma. Hata hivyo, ingali kubainika kuhusu ikiwa atashiriki katika Misa ya Ijumaa Njema au la.Kanisa hilo lina karibu washiriki 1.4 bilioni kote duniani.

  • Tags

You can share this post!

Monica Etot aokoa Kisumu All Starlets mikononi mwa Thika...

Raila asitisha maandamano

T L