• Nairobi
  • Last Updated May 13th, 2024 7:02 PM
Putin ashambulia Ukraine Krismasi

Putin ashambulia Ukraine Krismasi

Mnamo Jumapili, Wakristo walipokuwa wakisherehekea Krismasi, vikosi vyake vilifanya mashambulio zaidi ya 40 ya roketi dhidi ya Ukraine, kulingana na taarifa iliyotolewa na jeshi la taifa hilo.

Hapo jana Jumatatu, wanajeshi watatu wa Urusi waliuawa baada ya kuangukiwa na mabaki ya droni ya Ukraine iliyodunguliwa na vikosi vya Urusi wakati ilipokuwa ikishambulia kambi moja ya wanajeshi hao katika eneo la Saratov, nchini Urusi.

Kulingana na Wizara ya Ulinzi ya Urusi, hilo ndilo lilikuwa shambulio la pili dhidi ya kambi hiyo mwezi huu wa Desemba.

Kwenye shambulio la kwanza, kambi hiyo ambayo iko umbali wa kilomita 730 kaskazini mashariki mwa Moscow, ilishambuliwa na droni nyingine kadhaa kutoka Ukraine mwanzoni mwa mwezi huu wa Desemba.

Urusi ilisema Ukraine ilifanikiwa kushambulia kambi zake mbili za jeshi siku hiyo kwa kutumia droni.

Mnamo Jumapili, Putin alisema kuwa yuko tayari kushiriki katika mazungumzo huku akiilaumu Ukraine na washirika wake wa Magharibi kwa kukosa kushiriki kwenye mazungumzo hayo.

Hata hivyo, Amerika imekuwa ikipuuzilia mbali kauli ya Putin kutokana na mashambulio ambayo Urusi imekuwa ikiendelea kutekeleza dhidi ya miundomsingi muhimu nchini Ukraine.

“Tuko tayari kuzungumza na kila mhusika ili kupata suluhu itakayokubalika na kila mmoja. Lakini wao ndio watakaofanya maamuzi hayo. Si sisi tunaokataa kushiriki kwenye mazungumzo,” akasema Putin kwenye mahojiano na kituo cha televisheni cha Rossiya 1.

Mshauri mmoja wa Rais Volodymyr Zelensky alisema kuwa Putin anafaa kubaini na kueleza ukweli kuwa Urusi ndiyo haitaki kushiriki kwenye mazungumzo hayo.

“Urusi ilianzisha mashambulio dhidi ya Ukraine na bado inaendelea kuwaua raia wasio na hatia,” akasema mshauri huyo, Mykhailo Podolyak, kupitia mtandao wa Twitter.

“Urusi haitaki kushiriki kwenye mashauriano, lakini inajaribu kuepuka kuwajibikia makosa yake.”

Hatua ya Putin kuivamia Ukraine mnamo Februari 24 imezua mzozo mkubwa wa kivita barani Ulaya tangu Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Vita hivyo pia vimeibua mvutano mkubwa zaidi baina ya Urusi na mataifa ya Magharibi.

  • Tags

You can share this post!

Ajali ya boti iliyowaua wawili ufuo wa Pirate’s...

Acha kunipa presha, Ruto amfokea Raila

T L