• Nairobi
  • Last Updated April 17th, 2024 6:55 PM
Raia wa Pakistan akamatwa kwa kumuua mkewe aliyezaa na mpango wa kando

Raia wa Pakistan akamatwa kwa kumuua mkewe aliyezaa na mpango wa kando

Na DAILY MONITOR

KAMPALA, Uganda

POLISI nchini Uganda wanamzuilia raia mmoja wa Pakistan anayedaiwa kumuua mkewe na kuficha maiti yake ndani ya shimo la majitaka.

Kulingana na maafisa hao, Waeed Taheed, mkazi wa Wilaya ya Mpigo, mwanzoni aliripoti kisa cha kupotea kwa mkewe Monica Nabukenya, 25, mnamo Julai 16, 2023.

Inaripotiwa kuwa Taheed, 45, alishuku kuwa Nabukenya hakuwa mwaminifu kwake na ndipo akampeleka mtoto wao wa umri wa miezi sita akafanyiwe uchunguzi wa DNA kubaini babake mzazi.

“Taheed aliamua kumpeleka mtoto huyo afanyiwe uchunguzi wa DNA na matokeo yakawa kwamba yeye sio babake halisi,” taarifa ya polisi ikasema.

Mwanamume huyo aliporejea nyumbani ndipo akamuua mkewe na kutupa mwili wake ndani ya tangi la majitaka na kulifunika kwa mchanga kidogo.

“Baada ya kumhoji, polisi walimwagiza mshukiwa awapeleke nyumbani kwake. Walipowasili walikabiliwa na harufu ya maiti kutoka kwa shimo la majitaka. Baada ya kuhojiwa, Taheed alikubali kwamba alimuua mkewe kwa sababu matokeo ya DNA yalionyesha yeye sio baba wa mwanawe,” polisi wakasema.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kalagala, kilichoko viungani mwa mji wa Kayabwe, Richard Ddumba, alisema wanandoa hao wamekuwa wakiishi maisha yenye usiri hadi juzi alipopata habari kwamba wamezozana kuhusu suala la baba mtoto mwenye umri wa miezi sita.

“Kile ambacho nafahamu ni kwamba, wanandoa hao walikuwa na mtoto mmoja. Na mwanamume huyo alipopata habari kwamba mwanamume mwingine ndiye baba halisi wa mtoto huyo, alimpeleka mtoto kufanyiwa uchunguzi wa DNA kubaini kuwa yeye sio babake mzazi,” akasema.

Ddumba alisema Taheed alikuja kwake miezi minne iliyopita akimwambia angetaka kumtaliki mkewe.

Inadaiwa kuwa mwanamume huyo aliwasilisha kesi ya talaka mahakamani lakini hadi wakati alipomuua mkewe, kesi hiyo haikuwa imekamilika.

Tafsiri: CHARLES WASONGA

  • Tags

You can share this post!

Yuko wapi mume wangu, Babu Owino? Fridah Ongili ataka...

Familia ya Babu Owino yakita kambi katika kituo cha polisi...

T L