• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 1:05 PM
Familia ya Babu Owino yakita kambi katika kituo cha polisi cha Wang’uru

Familia ya Babu Owino yakita kambi katika kituo cha polisi cha Wang’uru

NA GEORGE MUNENE

FAMILIA ya Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino imekita kambi katika kituo cha polisi cha Wang’uru katika Kaunti ya Kirinyaga ikishinikiza aachiliwe.

Kando na familia, marafiki wa Bw Owino pia wako hapo wakishinikiza aachiliwe.

Mke wa mbunge huyo, Bi Fridah Ongili ameripoti kwamba mume wake anazuiliwa katika kituo hicho kilichoko Mwea, Kaunti ya Kirinyaga.

Bw Owino alikamatwa mnamo Jumanne usiku alipotua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) Nairobi akitoka jijini Mombasa.

Fridah amesema amezuiwa kumuona mume wake kwa sababu polisi wamewafurusha nje wanafamilia.

Ingawa hivyo, amethibitisha kwamba mume wake yuko katika kituo hicho.

Afisa wa polisi aifurusha familia ya Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino iondoke katika kituo cha polisi cha Wang’uru; mke wake Bi Fridah Ongili asema kiongozi huyo anazuiliwa hapo. PICHA | GEORGE MUNENE

Ana hofu huenda mume wake akahamishwa kutoka kituo hicho na kupelekwa pahali fulani kusikojulikana.

Anawataka viongozi wa Azimio La Umoja-One Kenya kuhakikisha anaachiliwa huru.

“Tuna habari kwamba huenda akahamishwa, ninamuomba Mungu kwamba mume wangu atabakia hapa. Ombi langu kwa kiongozi wa Azimio Raila Odinga ni kwamba afanye awezalo kumsaidia mume wangu. Serikali ninaiambia wazi inamshikilia mume wangu kinyume cha sheria. Ninachotaka kwa sasa ni kumpa mume wangu chakula na kuhakikisha kwamba yuko salama,” amesema Bi Ongili.

  • Tags

You can share this post!

Raia wa Pakistan akamatwa kwa kumuua mkewe aliyezaa na...

JURGEN NAMBEKA: Wakuu Mombasa watafute jibu kwa wanaozurura...

T L