• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 12:38 PM
Raia wa Zambia kumjua mshindi wa urais wikendi hii

Raia wa Zambia kumjua mshindi wa urais wikendi hii

Na AFP

LUSAKA, Zambia

RAIA wa Zambia, Alhamisi walipiga kura kumchagua Rais mpya, wabunge na madiwani, katika uchaguzi ambao ulisheheni ushindani mkali kati ya Rais wa sasa Edgar Lungu na kiongozi wa upinzani Hakainde Hichilema.

Shughuli za kuhesabu kura zilianza baada tu ya vituo vya upigaji kura kufungwa huku mshindi akitarajiwa kutangazwa rasmi Jumamosi au Jumapili.

Pia kuna wawaniaji wengine 14 waliojitosa debeni wakijaribu bahati yao kuingia ikulu.

Lungu, 64 mara hii anakabiliwa na mtihani mkubwa wa kusalia uongozini, akiwa anamenyana na Hichilema kwa mara ya tatu kwenye uchaguzi mkuu.

Hichilema, 59, ambaye amewania uchaguzi huo mara sita, amepigiwa upatu kutwaa ushindi na matokeo ya kampuni mbalimbali za utafiti.

Mwaniaji huyo aliingia katika muungano na vyama 10 vya upinzani na ana nafasi nzuri ikizingatiwa alipoteza kwa mwanya wa kura 100,000 katika uchaguzi wa 2016.

Mshindi wa kiti cha Urais lazima apate zaidi ya asilimia 50 ya kura na atakuwa pazuri kutekeleza sera zake iwapo chama chake kitashinda viti vingi vya ubunge.

Rais Lungu anawania kupitia chama cha Patriotic Front (PF) huku Hichilema akiwa katika muungano wa United Party for National Development (UPND).

You can share this post!

Karua aongoza Mlima kujipanga

Visa vya wizi wa pikipiki za bodaboda vyaongezeka Witeithie