• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Uganda italinda Urusi – mwanawe Museveni

Uganda italinda Urusi – mwanawe Museveni

KAMPALA, Uganda

MWANAWE Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Muhoozi Kainerugaba, ametangaza kuwa nchi yake itatuma wanajeshi kulinda Urusi ikiwa itavamiwa na mataifa ya Magharibi.

“Niite mtetezi wa Putin, lakini sisi, Uganda tutatuma wanajeshi kutetea Urusi ikiwa itatishiwa na mabeberu,” Kainerugaba akasema kupitia Twitter.

“Mataifa ya Magharibi yanapoteza muda wake mwingi na propaganda zake za kutetea Ukraine,” akaongeza Jenerali huyo wa jeshi la nchi kavu nchini Uganda na mfuasi mkubwa wa Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Kainerugaba, ambaye hupenda kutoa kauli zenye utata kupitia Twitter kuhusu masuala mbalimbali, mapema mwezi Machi, alitangaza kuwa atawania urais katika uchaguzi mkuu wa Uganda.

Mnamo Alhamisi alitangaza kuundwa kwa kituo cha televisheni na redio chini ya nembo yake, MK, kinachoongozwa na msemaji wa zamani wa jeshi la Uganda.

Kainerugaba alisema kituo hicho cha televisheni kitatuma wanahabari wake kutembelea Urusi.

Kama afisa wa kijeshi, Kainerugaba amepigwa marufuku, chini ya Katiba ya Uganda, kutoa taarifa kiholela kuhusu nchi huru au sera za kigeni.

Uganda imekuwa ikisusia upigaji kura katika Umoja wa Mataifa (UN), kuhusu suala la uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Aidha, ilisusia shughuli kama hiyo Februari 24 wakati wa maadhimisho wa mwaka moja tangu uvamizi huo, ambapo wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) walitaka Urusi iondoe wanajeshi wake nchini Urusi.

Rais Museveni amewahi kutetea uhusiano wa nchi yake na Rais Putin.

“Tunawezaje kumchukua mtu ambaye hajawahi kutudhuru,” akasema Julai mwaka jana Waziri wa Kigeni wa Urusi Sergei Lavrov alipozuru Afrika kusaka uungwaji mkono kwa vita vya Urusi nchini Ukraine.

Urusi imekuwa na uhusiano wa karibu na Afrika kwa miaka mingi baada ya kupiga jeki juhudi za nchi kadha za kupigana na serikali za kikoloni.Kwa muda mrefu, wadadisi wa siasa za Uganda wameamini kuwa Kainerugaba anaandaliwa kumrithi babake mwenye umri wa miaka 78, ambaye ameongoza nchi hiyo tangu 1986.

Lakini baadhi ya kauli ambazo jenerali huyo hutoa kupitia Twitter zimeisababishia Uganda matitizo ya kidiplomasia.

Baada ya Kainerugaba kutisha, kupitia Twitter, kwamba atavamia Kenya, Rais Museveni aliahidi kuwa atamdhibiti mwanawe na kumwonya dhidi ya kutoa kauli nzito kama hizo kupitia mtandao huo.

  • Tags

You can share this post!

CJ Koome kuteua majaji watakaoamua hatima ya CASs

Wanajeshi waliotumwa DRC kukawia zaidi

T L