• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 12:18 PM
UN, AU wapongeza utawala kuondoa hali ya hatari

UN, AU wapongeza utawala kuondoa hali ya hatari

NA XINHUA

KHARTOUM, SUDAN

UMOJA wa Mataifa (UN), Umoja wa Afrika (AU) na Shirika la Maendeleo la IGAD, zimepongeza hatua ya utawala wa Sudan kuondoa hali ya hatari nchini na kuachilia huru wafungwa wa kisiasa.

Zimetaja hatua hiyo ya Mwenyekiti wa Baraza la Mpito Nchini Sudan, Abdel Fattah Al-Burhan (pichani), kama hatua nzuri itakayoweka mazingira bora ya kutatuliwa kwa mzozo wa kisiasa nchini humo kwa njia ya amani.

UN, AU na Igad zimetoa wito kwa wadau wote kuwa tayari kuketi katika meza ya mazungumzo kusuluhisha tofauti kati yao.

Chama cha National Umma Party, ambacho ni mojawapo ya muungano wa vyama vya upinzani, Freedom and Change Alliance, pia kilitaja kuondolewa kwa hali ya hatari kama hatua itakayojenga imani ya wananchi kuwa amani na uthabiti itapatikana nchini humo.

Sudan imezongwa na msukosuko wa kisiasa jeshi lilipotwa uongozi baada ya kumpindua aliyekuwa rais wa nchi hiyo Omar el Bashir mnamo Julai 2020.

  • Tags

You can share this post!

Ruto, Raila sasa ni nipe nikupe Pwani

Kinoti apeleka Haji kortini mzozo kati yao ukiumiza raia

T L