• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:09 PM
Urusi yaonya Ukraine isipokee ala nzito za vita

Urusi yaonya Ukraine isipokee ala nzito za vita

NA MASHIRIKA

MOSCOW, URUSI

URUSI imetishia kuongeza mashambulio yake nchini Ukraine ikiwa itapokea makombora ya masafa marefu kutoka kwa mataifa ya magharibi

“Iwapo makombora hayo yatapewa Ukraine, tutatumia silaha zetu kushambulia maeneo ambayo hatujawahi kulenga,” Rais Vladimir Putin alisema kwenye mahojiano Jumatatu.

Putin alisema hatua ya mataifa ya magharibi kuipatia Ukraine silaha zaidi itachelewesha tu kumalizika kwa vita kati yake na Ukraine na kuzorotesha hali ya kibinadamu.

Ukraine imesema kuwa tayari imepokea vifaa vya kudengua makombora kutoka kwa Denmark, Uingereza na Uholanzi ili kuisaidia kujilinda katika eneo la Bahari Nyeusi.

Haya yanajiri Uingereza ikisema itapeleka makombora ya msafa marefu nchini Ukraine.

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema kuwa taifa hilo limekuwa likishirikiana na Amerika kuhusu mikakati ya kuisaidia Ukraine kwa makombora aina ya MLRS, yenye uwezo wa kurushwa mbali.

Makombora hayo yana uwezo wa kurushwa hadi umbali wa kilomita 80.

Uingereza ilisema makombora hayo yataisaidia Ukraine pakubwa kuvikabili vikosi vya Urusi.

Wiki iliyopita, Amerika ilisema itaisaidia Ukraine na mashine za kisasa za kurusha makombora aina ya HIMARS.

Mitambo hiyo ina uwezo wa kurusha makombora kadhaa kwa wakati mmoja.

Hata hivyo, Rais Joe Biden wa Amerika alisema kuwa taifa hilo halitaisaidia Ukraine na mitambo inayoweza kurusha makombora hadi nchini Urusi.

Hii ni licha ya Ukraine kuendelea kuirai Amerika kuisaidia kwa mitambo yenye uwezo huo.

Lakini kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi wa Uingereza, Ben Wallace, alisisitiza kuwa lazima washirika wa Ukraine kutoka Magharibi waisaidie kwa silaha kwa njia zozote wawezavy” ili kuiwezesha kuikabili Urusi vilivyo.

“Uingereza inasimama na Ukraine kwenye vita hivi. Tutaongoza kwenye juhudi za kuisaidia kwa silaha za kivita inavyohitaji ili kuitetea himaya yake dhidi ya uvamizi dhidi yake,” akasema waziri huyo kwenye taarifa.

“Urusi inapobadilisha mbinu zake za kijeshi, lazima tuungane pamoja kuisaidia Ukraine. Mitambo hiyo ya kurusha roketi itaisaidia sana kuboresha juhudi zake kujilinda dhidi ya mashambulio yanayotekelezwa na vikosi vya Putin,” akasema.

  • Tags

You can share this post!

TIBA NA TABIBU: Kulegea, kuoza kwa meno inaweza kuwa dalili...

CHARLES WASONGA: Kipengee kinachowakinga fisadi katika...

T L