• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Wajumbe wa kongamano la AHAIC washiriki hafla ya matembezi siku ya kutotumia magari nchini Rwanda

Wajumbe wa kongamano la AHAIC washiriki hafla ya matembezi siku ya kutotumia magari nchini Rwanda

NA PAULINE ONGAJI

KIGALI, RWANDA

KONGAMANO la Kimataifa kuhusu ajenda ya afya barani Afrika (AHAIC 2023) litang’oa nanga rasmi Jumanne jijini Kigali, Rwanda.

Kongamano hili limeandaliwa kwa ushirikiano wa shirika la Amref Health Africa, Wizara ya Afya nchini Rwanda, Muungano wa Afrika na Africa CDC, lilitanguliwa na hafla ya matembezi kuambatana na siku rasmi ya kutotumia magari jijini humo, ambayo huadhimishwa Jumapili ya kwanza na ya tatu kila mwezi, kama mbinu za kuhakikisha jiji hili linasalia safi kimazingira na pia ili kukabiliana na maradhi yasiyosambaa (NCDs).

Haya yakiwa Makala ya tano, kongamano hili litaleta pamoja baadhi ya viongozi wakuu barani, wanasiasa, wavumbuzi, watafiti, wahudumu wa kiafya, miongoni mwa washikadau wengine katika sekta ya afya, ili kujadili mwelekeo wa kuunganisha masuala ya tabianchi na sera za kiafya.

Kama mojawapo ya mikutano mikuu ya kiafya mwaka huu, kongamano hili aidha litatoa jukwaa la kujadili masuala ambayo yameratibiwa kuzungumziwa katika bunge la Afya ulimwenguni, Bunge kuu la Unoja wa Mataifa (UNGA) na kongamano la 2023 la Umoja wa Mataifa kuhusiana na mabadiliko ya tabianchi, al-maarufu COP28 mwaka huu.

Tangu mwaka wa 2014, kongamano hilo ambalo huandaliwa kila baada ya miaka miwili limekuwa likihusisha washikadau katika masuala ya kiafya kutoka barani Afrika, ili kuzungumzia masuala ya afya, kuunda msingi wa ushirikiano wa mataifa yenye mapato ya chini, na kumarisha mifumo thabiti ya afya.

Kongamano la mwisho la AHAIC lilifanyika 2021 kwa njia ya mtandaoni kutokana na marufuku ya usafiri yaliyotokana na maradhi ya COVID 19 ambapo zaidi ya washiriki 3,000 walihusika.

Katika hafla hiyo, shirika la Amref Health Africa lilizindua tume huru ya kukagua hatua ambazo mataifa ya Afrika zimepiga katika kutimiza ndoto ya Afya kwa wote (UHC) kufikia mwaka wa 2030.

Hii ilifuatiwa na uchapishaji wa ripoti ya The State of UHC in Africa, iliyotoa kwa kina hatua ambazo serikali za Afrika zimechukua katika kutimiza UHC. Kongamano hili linatarajiwa kukamilika Alhamisi Machi 8.

  • Tags

You can share this post!

TEKNOLOJIA: Tecno yazindua simu aina ya Phantom V Fold

Arsenal watoka nyuma na kupepeta Bournemouth 3-2 katika EPL...

T L