• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 11:53 AM
Arsenal watoka nyuma na kupepeta Bournemouth 3-2 katika EPL ugani Emirates

Arsenal watoka nyuma na kupepeta Bournemouth 3-2 katika EPL ugani Emirates

Na MASHIRIKA

REISS Nelson alifungia Arsenal bao la ushindi katika mechi iliyoshuhudia viongozi hao wa jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) wakitoka nyuma kwa mabao mawili kwa nunge na kusajili ushindi wa 3-2 dhidi ya Bournemouth mnamo Jumamosi ugani Emirates.

Bournemouth walijiweka kifua mbele baada ya sekunde 9.11 pekee za mchezo kupitia kwa Philip Billing kabla ya kufungiwa bao la pili na Marcos Senesi katika dakika ya 57.

Hata hivyo, Arsenal walirejea mchezoni kupitia kwa Thomas Partey aliyecheka na nyavu katika dakika ya 62 kabla ya Ben White kusawazisha mambo kunako dakika ya 70 kisha Nelson akafunga goli la ushindi katika sekunde za mwisho.

Nelson aliyekuwa akichezea Arsenal kwa mara ya kwanza tangu Novemba 12, alivurumisha kombora kutoka hatua ya mita 23. Ushindi huo ulidumisha pengo la alama tano linalojivuniwa na Arsenal kati yao na nambari mbili Manchester City kileleni mwa jedwali la EPL.

Arsenal ambao sasa wanajivunia alama 63, walishuka dimbani wakiwa na presha ya kutokaribiwa na mabingwa watetezi Man-City waliopepeta Newcastle 2-0 ugani Etihad.

Bournemouth sasa wanavuta mkia wa jedwali la EPL kwa alama 21 sawa na Everton na Southampton waliokung’uta Leicester City 1-0.

Bao la Billing lilikuwa lake pili la haraka zaidi kuwahi kufungwa katika historia ya EPL baada ya Shane Long kupachikia Southampton baada ya sekunde 7.69 pekee dhidi ya Watford mnamo Aprili 2019.

Nelson alishuka dimbani dhidi ya Bournemouth akijivunia kusakata soka kwa dakika 64 pekee katika EPL msimu huu baada ya jeraha la paja kumweka nje kwa kipindi kirefu.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Wajumbe wa kongamano la AHAIC washiriki hafla ya matembezi...

Wanaraga Kabras na KCB waingia fainali Kenya Cup baada ya...

T L