• Nairobi
  • Last Updated April 17th, 2024 6:55 PM
Wakazi kupewa bangi baada kupokea chanjo

Wakazi kupewa bangi baada kupokea chanjo

Na MASHIRIKA

WATU wazima jijini Washington, Amerika, sasa wanaweza kuitisha msokoto wa bangi kama zawadi kwa kupokea chanjo ya Covid-19 hadi Julai 12.

Bodi inayosimamia matumizi ya Pombe na Bangi Washington ilitangaza Jumatatu kuwa, mpango huo kwa jina “Msokoto kwa kupokea Chanjo” utaanza kutekelezwa mara moja.

Katika kipindi hicho, wauzaji wa bangi walio na leseni eneo hilo wataruhusiwa kuwapa msokoto wa bangi wateja wao walio na umri wa kuanzia miaka 21, watakaopokea dozi yao ya kwanza au ya pili ya Covid-19 kutoka kliniki ya utoaji chanjo.

Wateja wataweza tu kuitisha msokoto wa bangi kutoka kwa wauzaji eneo hilo baada tu ya kupokea chanjo kulingana na bodi hiyo.

 

You can share this post!

Rais wa Ufaransa azabwa kofi na mkazi

CHAKIBU: Jivunio la Butula Boys kwa makuzi ya lugha