• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:55 AM
Wanajeshi wapindua serikali ya muda Sudan

Wanajeshi wapindua serikali ya muda Sudan

Na MASHIRIKA

WANAJESHI wametimua raia kutoka katika baraza la serikali ya mpito huku Waziri Mkuu, 65, akizuliwa.

Wizara ya habari jana ilisema kuwa Hamdok alikamatwa na wanajeshi baada ya kukataa ‘kushirikiana’ nao.Baadaye, mwenyekiti wa baraza la serikali ya mpito linaloongoza serikali ya Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, alitangaza kuvunja serikali na akatangaza hali ya tahadhari kote nchini.

Jenerali Abdel Fattah al-Burhan pia alitimua magavana wote huku akitangaza kuwa uchaguzi mpya wa wakuu wa majimbo utafanyika Julai 2023.Kumekuwa na mvutano kuhusu namna ya kugawa mamlaka kati ya wanajeshi na raia tangu kupinduliwa kwa serikali ya Omar al-Bashir mnamo Aprili 2019.

Raia wanataka wanajeshi wawakabidhi mamlaka. Jeshi, kwa upande mwingine, limeshikilia kuwa halitabanduka mamlakani.Sudan imekuwa ikiendeshwa na baraza la serikali ya mpito linaloongozwa na Fattah al-Burhan ambaye ni afisa wa jeshi.

Jana, afisi ya Waziri Mkuu, iliwataka raia wa Sudan kufanya maandamano makubwa kote nchini kushinikiza wanajeshi kurejesha raia serikalini na kumwachilia huru Abdalla Hamdok.Hamdok si mwanajeshi na anawakilisha raia katika serikali ya mpito.

Wanajeshi pia wanashikilia maafisa wa kiraia wanaohudumu katika serikali ya mpito.“Tunahimiza raia wote wa Sudan kupinga kwa kutumia mbinu za kila aina kurejesha serikali yao ambayo imenyakuliwa na wanajeshi,” ikasema taarifa kutoka afisi ya waziri mkuu.

  • Tags

You can share this post!

Maradhi ya Trakoma yanapofusha maelfu maeneo kame

Maji ya Ziwa Victoria yasababisha kansa, watahadharisha...

T L