• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 8:55 AM
Wananchi kuwa na usemi mkuu katika biashara ya pombe

Wananchi kuwa na usemi mkuu katika biashara ya pombe

Na RICHARD MUNGUTI

USHIRIKI wa umma katika utoaji leseni za kuweka mabaa utapewa kipau mbele kabla ya yeyote kuanza kuuza pombe, Taifa Leo imefahamishwa.

Kupitia mahojiano ya kipekee, Mbunge Mwakilishi wa Wanawake Kaunti ya Kirinyaga, Bi Jane Njeri Maina alisema pombe inaendelea kulemaza jamii kwa kasi na hatua za dharura zisipochukuliwa nchi hii haitakuwa na vijana.

Bi Maina, 29, alisema maduka yanayouza pombe hatari za Wines & Spirits zimechangia pakubwa katika uzamishaji vijana.

Mbunge huyo aidha alieleza kusikitishwa kwake kwa maduka hayo, akisema yanauza pombe ya bei rahisi ambayo imechangia pakubwa kuporomoka kwa maisha ya vijana.

Pombe hii, aliongeza kusema inauzwa Sh30 ama Sh50 na iko na madhara makubwa kwa afya.

“Kabla ya mfanyabiashara kuanza kuuza pombe lazima wakazi wa kila eneo waulizwe maoni yao. Wananchi watakuwa wanaidhinisha kuwekwa kwa mabaa au la,” Bi Maina alifafanua Jumapili.

Bi Maina ambaye pia ni wakili amefichua kwamba amechangia pakubwa katika utunzi wa sheria kudhibiti utengenezaji na uuzaji pombe.

“Wananchi ndio watakuwa na usemi mkuu katika uuzaji wa pombe katika kila eneo nchini,” Bi Maina alidokeza.

Naibu Rais Rigathi Gachagua amesisitiza kuwa hatalegeza kamba oparesheni dhidi ya pombe haramu Mlima Kenya, akisema maeneo mengine ya nchi pia yatafuata mkondo huo.

  • Tags

You can share this post!

Mung’aro aahidi kuboresha huduma za afya mashinani 

Walanguzi 3 wa dawa za kulevya wakamatwa

T L