• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Watumishi wa umma wanyimwa ladha ya TikTok

Watumishi wa umma wanyimwa ladha ya TikTok

NA MASHIRIKA

PARIS, UFARANSA

UFARANSA ndilo taifa la hivi punde kupiga marufuku TikTok kwenye simu za watumishi wa umma.

Maafisa wanasema apu hiyo ni hatari kwa sababu haina kinga thabiti na hivyo ni rahisi kwa data za watumiaji kudukuliwa.

Marufuku hayo yanaanza kutelekezwa mara moja, imesema Wizara ya Uimarishaji wa Sekta ya Umma na Utumishi wa Umma kupitia Twitter. Aidha marufuku hayo yanaathiri pia Instagram na jukwaa la filamu la Netflix.

Mataifa mengine yaliyochukua hatua kama hizo ni Amerika, Ujerumani, Uingereza na Kamisheni ya Ulaya ambapo TikTok inakabiliwa na kibarua kizito kujisafisha.

  • Tags

You can share this post!

Pasta anayehusishwa na vifo vya watoto akana mashtaka

DOUGLAS MUTUA: Putin ni papa nayo ICC dagaa?

T L