• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:15 PM
Zimbabwe yaruhusu biashara ya bidhaa zilizotengenezwa kwa bangi

Zimbabwe yaruhusu biashara ya bidhaa zilizotengenezwa kwa bangi

NA KITSEPILE NYATHI

SERIKALI ya Zimbabwe imeruhusu, kwa mara ya kwanza kuuzwa kwa bidhaa za kimatibabu zilizotengenezwa kwa kutumia bangi huku taifa hilo la Afrika Kusini likilenga kufaidi kutokana na sekta hiyo yenye thamani ya Sh148.5 bilioni.

Shirika la Kudhibiti Dawa Nchini Zimbabwe (MCZ) limetoa nafasi kwa wazalishaji, watengeneza na wauza bidhaa zilizotengenezwa kwa bangi kutuma maombi ya leseni za kuendesha shughuli hizo.

Zimbabwe ilihalalisha bangi kwa shughuli za kibiashara na kutengeneza dawa mnamo 2019.

Hata hivyo, hakuna hatua ambayo imechukuliwa kuendeleza shughuli hizo ili kuiletea taifa hilo masikini mapato, Zimbabwe pia inazongwa na mzigo mkubwa wa madeni na kudorora kwa uchumi kufuatia kupungua kwa sarafu yake dhidi ya sarafu za kigeni.

Mnamo Jumanne, Julai 26, 2022, MCZ ilitoa kanuni zitakazozingatiwa kusimamia uwekezaji katika sekta biashara ya bidhaa za bangi nchini Zimbabwe.

Taifa hilo limewekewa vikwazo vya kiuchumi na mataifa ya Magharibi, kutokana na rekodi yake mbaya katika udumishaji wa haki za kibinadamu kando na ukandamizaji wa viongozi wa upinzani.

Sasa inalenga kufaidi kutoka na soko ya bangi na bidhaa zake katika ngazi za kimataifa.

Zimbabwe, ambayo inaongozwa kwa uzalishaji wa tumbaku, sasa anataka kuelekeza juhudi zake katika ustawishaji wa sekta ya bangi, kutokana na kampeni inayoendeshwa ulimwenguni dhidi ya bidhaa za tumbaku.

Mwishoni mwa mwaka wa 2021, Zimbabwe iliuza tani 30 ya bangi aina ya “hemp” nchini Uswisi.

Mnamo Mei 2022, Rais Emmerson Mnangagwa alizindua shamba la kukuza bangi ya kutumiwa kutengeneza dawa na kiwanda cha kutungeneza bangi hiyo.

Kampuni hiyo inamilikiwa na kampuni ya dawa ya Swiss Bioceutical Limited.

Wakati huo huo, Rais Mnangagwa alifichua kuwa kampuni 57 zimepewa leseni ya kuzalisha bangi na kampuni 15 kati yazo zimeanza kufanya kazi.

Watetezi wa matumizi ya bidhaa za bangi wanasema kuwa zinaweza kutumia kudhibiti matatizo ya kiafya kama vile; uchungu kupita kiasi, muwasho, kifafa, msongo wa kimawazo, miongoni mwa matatizo mengine.

Hata hivyo, Zimbabwe bado imepiga marufuku matumizi ya bangi kwa ajili ya burudani. Maelfu ya watu wamekamatwa mwaka huu kwa tuhuma za kukuza aina hiyo ya bangi, katika jitihada za nchi hiyo kupiga vita matumizi mabaya ya dawa za kulevya miongoni mwa vijana.

TAFSIRI: CHARLES WASONGA 

  • Tags

You can share this post!

Wabunge 12 wajaribu kuvunja laana ya kura

Walionusurika ajali ya Mto Nithi wasimulia tukio hilo

T L