• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 11:28 AM
Jinsi ya kuandaa mlo bora bila kutumia mafuta

Jinsi ya kuandaa mlo bora bila kutumia mafuta

Na PAULINE ONGAJI

Kutokana na sababu za kiafya, kuna baadhi ya watu ambao hawatumii chakula kilichopikwa kwa mafuta ya kukaanga.

Kutokana na sababu hii, kunao baadhi ya watu ambao wamelazimika kula vyakula vya kuchemsha tu.
Mara nyingi, chakula hiki hakifurahishi. Lakini je wajua kwamba inawezekana kupika chakula bila kutumia mafuta ya kukaanga na upate matokeo mema? Vidokezi hivi vitakusaidia:

· Kukaanga: Unapofanya hivi, badala ya kutumia mafuta au siagi waweza tumia maji kidogo au supu ya mboga huku ukiendelea kuongeza muda unavyosonga.

· Kuoka: Katika mbinu hii ya mapishi waweza tumia rojo ya matunda badala ya mafuta au siagi. Baadhi ya aina za rojo mwafaka katika mapishi haya ni ya ndizi, njugu au tende.

· Kuchoma: Badala ya kupaka nyama au mboga zako mafuta kabla ya kuzichoma, waweza zitumbukiza kwenye supu ya mboga au kwenye mchanganyiko wa viungo.

· Badala ya kukaanga vyakula kwa mafuta mengi, waweza oka. Kwa rojo zinazoundwa kwa kutumia siagi au mtindi, waweza tumia rojo ya maharagwe, pojo au mboga kama vile karoti.

· Kwa rojo inayotumika kwenye saladi, waweza changanya siki, viungo pamoja na juisi ya matunda badala ya kutumia krimu, mtindi au siagi.

  • Tags

You can share this post!

Leteni hao Uganda, chipukizi wa Kenya wafoka baada ya...

Kidosho na shemeji waingia mitini baada ya kunaswa na mzee...

T L