• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 9:50 AM
KWA KIFUPI: Chanjo ya corona inaisha makali baada ya miezi sita – WHO

KWA KIFUPI: Chanjo ya corona inaisha makali baada ya miezi sita – WHO

Na LEONARD ONYANGO

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) limethibitisha kuwa chanjo za corona zinazotolewa humu nchini na kote ulimwenguni, zinapungua makali mwilini baada ya miezi sita.

Ripoti ya WHO inaonyesha kuwa chanjo ya corona inapungua makali kwa asilimia nane miongoni mwa watu wa chini ya umri miaka 50. Chanjo hiyo inaishiwa makali kwa asilimia 10 miongoni mwa watu wa zaidi ya miaka 50.

Nchi 126 duniani, ikiwemo Kenya, tayari zimeidhinisha kutolewa kwa dozi ya tatu ili kuongeza makali ya chanjo mwilini.

Lakini shirika la WHO linashauri nchi kuwapa chanjo wagonjwa na wazee na kuwaacha vijana.

“Kuna watu wengi duniani ambao hawajapata hata dozi moja ya chanjo ya corona. Hivyo, haitakuwa vyema kuwachanja watu dozi ya tatu ilhali kuna wengine ambao hawajapata chanjo.

“Dozi ya tatu itolewe tu kwa watu walio hatarini zaidi kama vile wazee, wagonjwa wa kisukari, kansa kati ya maradhi mengineyo,” ikasema ripoti ya WHO.

Mwenyekiti wa Jopokazi la Utoaji wa Chanjo ya Corona, Dkt Willis Akhwale, anasema kuwa Kenya itaanza kutoa dozi ya tatu kwa wagonjwa na wazee kuanzia Januari, mwaka ujao.

Utafiti unaonyesha kuwa dozi ya tatu ya chanjo ya AstraZeneca inawezesha mwili kushinda aina mpya ya virusi vya corona, Omicron.

  • Tags

You can share this post!

MUME KIGONGO: Wanaume wastahili chanjo ya HPV, madaktari...

Namna ufalme wa Mwendwa katika soka nchini ulivyoporomoshwa...

T L