• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 3:46 PM
‘Taste of Nairobi’ yatoa fursa ya kipekee hoteli zikiandaa mlo mtamu

‘Taste of Nairobi’ yatoa fursa ya kipekee hoteli zikiandaa mlo mtamu

Na WANGU KANURI

KAMPUNI ya Mastercard ikishirikiana na mtandao wa EatOut na kampuni ya vileo ya Singleton ilizindua kampeni ya kuonyesha vyakula aina aina katika baadhi ya hoteli jijini Nairobi.

Kampeni hiyo iliyopagazwa ‘Taste of Nairobi’ imenuia kupiga jeki sekta ya hoteli licha ya kukumbwa na misukosuko iliyosababishwa na janga la corona.

Masharti ya Wizara ya Afya kwa wamiliki wa hoteli ili kuzuia uenezi wa Covid-19 yalisambaratisha sekta hiyo huku baadhi ya hoteli zikilazimika kufungwa na nyingine zikiwapiga kalamu wafanyakazi wake.

Lakini sasa kampeni hiyo ililenga kuwapa wapishi na wataalamu wa vyakula fursa ya kushabikia na kuonyesha ubunifu wao kupitia vyakula wanavyopika katika hoteli mbalimbali jijini Nairobi.

“Kupitia Taste of Nairobi tunapata nafasi ya kujitangaza kwa dunia na kuzionea fahari hoteli zetu zilizoko katika maeneo tofauti jijini Nairobi,” akasema Meneja Mkuu wa EatOut, Joy Wairimu.

Ushirikiano wa kampuni hizo tatu umejikita katika hoteli 12 ambazo ni About Thyme, Ate, Beit e Selam, Boho Eatery, Copper at The Social House, Cultiva, Hero at Trademark, Hob House, Inti Nikkei, Inca at The Social House, Talisman, The Local Grill, Tapas Westgate, Mawimbi Seafood, The Other Room at The Social House na Zen Garden.

Kampeni hiyo iliyoanza Novemba 4, 2021, itaendelea hadi Desemba 31 na kuwafaa watakaoshiriki kwenye kampeni hiyo kwa chajio na kileo.

“Kupitia Taste of Nairobi tunakumbushwa kuwa upishi wa chakula na sanaa ya maandalizi yake huweza kuboresha maisha ya watu na pia kuendeleza biashara,” akaongeza Meneja wa Mastercard katika kanda ya Afrika Mashariki Bw Shehryar Ali.

  • Tags

You can share this post!

Nasa ulikuwa muungano wa kusaka uongozi 2017, asema Junet

SHINA LA UHAI: Kipindi kigumu kwa walio na HIV na TB

T L