• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 10:55 AM
Aunda programu ya kuvumisha burudani

Aunda programu ya kuvumisha burudani

Na MAGDALENE WANJA

Mnamo mwezi Aprili mwaka 2020, serikali ilikuwa imeanza kuweka sheria mpya za kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 mojawapo ikiwa marufuku ya usafiri na burudani.

Bw Emmanuel Nabuora alijipata pagumu kutokana na uamuzi huo kwani alikuwa amezoea sana kusafiri na kuhudhuria sherehe.

Marufuku ya usafiri ilipowekwa alikuwa nyumbani kwao mjini Kitale ambako kama miji mingine nchini kulikuwa kumeadhirika.

Nabuora ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa zamani wa Chama cha Ushirika wa Biashara katika Kaunti ya Trans Nzoia alijihisi mpweke sana kwani alikuwa maezoea kusafiri sio tu nchini mbali ata mataifa mengine.

“Nilianza kutafuta mtandaoni iwapo ningeweza kupata angalau ata sherehe zinazofanyika kwenye mtandao ila sikupata chochote katika eneo langu,” alisema Nabuora.

Hii ilimpa wazo la jinsi angeweza kuanzisha program ambayo ingeweza kuwaleta pamoja watu wanaosaka burudani ama kujivinjari mtandaoni.

Baada ya kuwaza, aliweza kutengeneza programu kwa jina PARTEUP, ambayo ingewafaa sana watu wapendao burudani.

Kwa kutumia Sh800,000  program hio ilikuwa imekamilika na ilikuwa tayari kuwafaa wanaburudani na wanabiashara katika miji mikuu nchini.

Program hii inapatikana katika Google Play. Programu hii ina manufaa kwa watu wanaopanga sherehe haswa za kiburudani, wamiliki wa vilabu na wageni wanaozuru mji Fulani kwa mara ya kwanza ili kuwaelekeza katika maeneo ya burudani.

“Programu hii pia inawapa nafasi watu kuwasiliana, kuuza na kununua na kuagiza vyakula na vinywaji kutoka maeneo yaliko karibu,” aliongeza Nabuora.

Programu hii pia inawapa nafasi watu kujifunza tamaduni za watu wa jamii mbali mbali kupitia maelekezo ya kuhudhuria sherehe mbali mbali.

“Wanabiashara pia wana nafasi ya kupata majibu kuhusu huduma zao kutoka kwa wateja kupitia program hii na hivyo kuwasaidia katika kufanya huduma zao ama bidhaa kuwa bora zaidi,” aliongeza Bw Nabuora.

Programu hii pia ina uwezo wa kuunda nafasi zaidi za kazi kwa wanaoitumia kwani ina nafasi zaidi kutokana na idadi kubwa ya watu wanaoweza kuitumia kwa wakati mmoja.

Kupitia program hii, waandalizi wa sherehe wanaweza kupeperusha matukio moja kwa moja.

You can share this post!

‘Simu ya mwenzako sumu’

Ziara ya Waiguru kwa Raila yazua gumzo mitandaoni