• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Baadhi ya visababishi vya kiungulia

Baadhi ya visababishi vya kiungulia

NA MARGARET MAINA

[email protected]

KIUNGULIA humfanya mtu ahisi kana kwamba kuna mwasho kifuani.

Chakula tunachokula hupitia kinywani mwetu hadi kwenye mirija inayojulikana kama umio. Kinapitia uwazi ulio kati ya umio na tumbo. Ufunguzi unafungwa mara tu chakula kinapopita. Iwapo umio haufungi, basi asidi iliyotengenezwa tumboni huingia kwenye umio na kusababisha kiungulia.

Ni nini husababisha kiungulia?

Baadhi ya visababishi vikuu vya kiungulia ni:

Kula kupita kiasi – Iwapo mtu anakula chakula chenye pilipili nyingi basi anaweza kuugua kiungulia.

Ukosefu wa chakula pia husababisha kiungulia.

Mimba pia inaweza kuzidisha kiungulia.

Mafadhaiko pia yanaweza kusababisha kiungulia.

Mavazi ya kubana pia husababisha usumbufu mwingi unaopelekea kiungulia.

Uvutaji sigara ni sababu nyingine ya hali hii ya kiafya.

Kahawa na vinywaji vyenye kafeini pia vinaweza kusababisha.

Pombe.

Bidhaa za nyanya.

Vyakula vyenye viungo au mafuta.

Vitunguu.

Uzito kupita kiasi.

Mambo mengi husababisha kiungulia, kama vile mtindo wa maisha usiofaa, tabia ya kula, kuvuta sigara, ugonjwa wa hernia, baadhi ya vyakula, baadhi ya dawa, unene au hata msongo wa mawazo. Mara tu unapougua kiungulia, ni vyema kutafuta tiba madhubuti za nyumbani ili kuponya reflux ya asidi na kuizuia isizidi kuwa mbaya.

Soda ya kuoka

Soda ya kuoka inafaa kwa kila aina ya tiba za nyumbani. Weka nusu ya kijiko cha chai cha soda ya kuoka ndani ya kikombe nusu cha maji baridi, kisha unywe ili kupunguza hisia za moto zinazosababishwa na kiungulia.

Maji

Kunywa maji safi iwezekanavyo unapohisi kiungulia. Hii pia huenda kwa hali wakati dalili yako si mbaya.

Siki ya Apple Cider

Changanya vijiko vya siki ya apple cider na maji moto kiasi, na kunywa wakati unakula chakula cha jioni.

Mbegu za shamari

Mbegu ya shamari ni mimea yenye harufu nzuri ambayo husaidia mmeng’enyo wa chakula. Kutafuna kijiko nusu cha mbegu za shamari huthibitisha manufaa na kusaidia kupunguza kiungulia.

Badilisha mazoea yako ya kula

Lishe yenye afya: Kula vyakula vyenye nyuzinyuzi nyingi zaidi kama vile shayiri, tufaha, parachichi na mboga. Chokoleti, mnanaa, kahawa, pombe na vyakula vya viungo hufanya dalili zako za kiungulia kuwa mbaya zaidi. Epuka sukari na wanga.

Njia ya Kula: Ni busara kugawanya milo yako ya kila siku katika milo midogo kadhaa, badala ya milo miwili au mitatu mikubwa.

Baada ya Kula: Ni vizuri kwako kutembea kwa muda. Epuka kula vitafunio kabla ya kulala.

Kiungulia mara nyingi hutokea katika maisha haya ya kisasa. Watu wengi hawana wakati wa kula chakula kinachofaa. Hii husababisha shida ya utumbo na kiungulia.

  • Tags

You can share this post!

Mkate wa shayiri na ndizi

Je, unafahamu kwamba kuogelea kuna faida tele?

T L