• Nairobi
  • Last Updated April 15th, 2024 2:58 PM
Frankie, Maureen wakumbatiana kwa mara ya kwanza baada ya kutibuana vibaya 2019

Frankie, Maureen wakumbatiana kwa mara ya kwanza baada ya kutibuana vibaya 2019

NA FRIDAH OKACHI

MWANAKOTENTI Maureen Waititu alikutana kwa mara ya kwanza na Frankie Kiarie maarufu Frankie Just Gym It baada ya kuweka tofauti zao kando na kushughulikia maslahi ya watoto wao wawili.

Wawili hao walikutana kwenye bethidei ya mwana wao ambaye anafahamika kama Lexi ambaye amehitimu umri wa miaka minane.

Frankie Just Gym It anafahamika kwa kazi yake ya kufanya mazoezi ya mwili.

Kwenye video iliyochapishwa kwenye ukurasa wa Frankie Just Gym, Bi Waititu alikumbatiana naye, ishara tofauti zao ziliisha.

Frankie aliendelea kuwakumbatia wazazi wa aliyekuwa mke wake na baadaye akaungana na mwanawe Lexi.

“Wikendi tulimsherekea huyu shujaa wetu. Heri njema ya kuzaliwa kwake. Amehitimu miaka minane sasa. Unapendeza Lexi! Unalete furaha na tabasamu maishani mwetu. Huu ni mwaka wa matukio makuu na kukua. Tunakupenda,” alichapisha Frankie.

Kwenye ukurasa wake, Maureen alichapisha picha kadhaa akiwa na wanawe akisherehekea siku hiyo, famiia yake ilijumuisha mamaye, babaye na wanawe wote wakivalia mavazi yenye rangi ya samawati giza.

“Mzee wa busara alisema, huwezi chagua familia yako. Hawa ni zawadi kutoka kwa Mungu,” alichapisha Waititu.

“Kumbukumbu kubwa kwa watoto wadogo, Lexi unapendwa na kuthaminiwa. Huyu ni mwanangu wa kiume,” aliendelea kuchapisha.

Mwanakotenti huyo, Oktoba 2, 2023 alimpongeza baba wa watoto wake Frankie kwa kufungua kituo cha mazoezi ya mwili kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Muundaji wa maudhui huyo alisema anajivunia Frankie kabla ya kuumuliza ikiwa angechangia zaidi katika malezi ya watoto.

“Hongera Frankie, ninajivunia sana bidii na juhudi zako unapofungua kituo chako cha mazoezi ya mwili. Sasa mchango wako kwa watoto utaongezeka,” alichapisha Maureen.

Mwaka wa 2019 wawili hao waliachana na kurushiana cheche za maneno kupitia mtandao ya kijamii Maureen akisusia kupokea usaidizi wa kuwalea wanawe kutoka kwa Frankie ambaye alishikana na soshiolaiti na wakili Corazon Kwamboka.

  • Tags

You can share this post!

Afisa wa DCI azuiliwa akidaiwa kupora simu ya mwanamke...

DPP kutathmini upya kesi ya wizi wa Sh122 milioni dhidi ya...

T L