• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
Kuna wakati nilitaka kujitoa uhai sababu ya jumbe nyingi za chuki – Azziad Nasenya

Kuna wakati nilitaka kujitoa uhai sababu ya jumbe nyingi za chuki – Azziad Nasenya

NA FRIDAH OKACHI

MWANAKONTENTI Azziad Nasenya amewashukuru mashabiki na familia yake kumjulia hali, baada ya kuzungumzia jinsi alivyokabiliana na msongo wa mawazo ambao ulimfanya kuwazia kujitoa uhai miaka mitatu iliyopita, wakati video zake kusambaa mitandaoni.

Kwenye ukurasa wake wa Facebook, ameweka wazi suala hilo lilifanyika miaka mitatu iliyopita akiwa tineja ambaye alikuwa akifanya jambo lililokuwa likimfurahisha wakati huo.

“Asante kwa kila mmoja anayenijulia hali kwa sasa, nipo sawa. Hapa nchini ni vizuri kufahamu ukipatwa na msongo wa mawazo hakuna anayehusika kukusaidia kwa wakati huo,” alisema Azziad.

Katika mahojiano na Dr Ofweneke, Azziad alisema alipatwa na wazo la kujitoa uhai baada ya video zake kusambaa kwenye mitandao kutokana na jinsi alivyokuwa akinengua ngoma ya Mejja na Femi One, Utawezana.

Azziad alisema mashabiki walianza kumchukia baada ya kutazama ngoma hiyo na kuzua mjadala ambao ulimzidishia mawazo ya kujitoa uhai. Hata hivyo. muda ulivyosonga, mashabiki hao walianza kumkubali.

“Wakati huo nilikuwa nikiishi katika ghorofa ya 4 na nilipokuwa nikitoka nje, wazo la kujitoa uhai lilikuwa likinijia. Maombi yangu  kwa Mungu yakazidi mawazo hayo mabaya,” alisimulia Azziad.

“Maoni kuhusu video hiyo yalibadilika baada ya siku moja na nusu, na nikaanza kupokea ukosoaji kutoka kwa baadhi ya mashabiki, nilijaribu kuvumilia nikashindwa. Nakumbuka nilikuwa peke yangu, nilikuwa nikilia, nikatoka nje kwenye roshani  ‘balcony’ nikatazama chini na nikaongea na Mungu wangu nikamuuliza, je Mungu hapa ndipo  ulitaka niende?” alisimulia mwanahabari huyo.

Mwanakontenti huyo alianza kutafakari wengi wa marafiki wake wa karibu wakikosa kumjali na kufahamu iwapo atakufa na kupata ushauri kutoka kwa watu wake wa karibu ambao walimpa tumaini.

Hatimaye ameweza kufaulu baada ya kukabiliana na msongo huo wa mawazo.

Mapema 2023, mwanahabari huyo mwenye umri wa 23, alipata kazi katika Wizara ya Michezo kutokana na bidii na kisomo chake.

  • Tags

You can share this post!

Kiongozi wa wengi Kiambu nje, Karani wa Machakos akiponea

Serikali ya UDA inasakamwa na ushindi walioniibia, Raila...

T L