• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 8:50 AM
Oga Obinna: Namuombea Willy Paul arudi kwa Yesu, muziki wa kidunia haumfai

Oga Obinna: Namuombea Willy Paul arudi kwa Yesu, muziki wa kidunia haumfai

Na MWANDISHI WETU

MWANAHABARI Steve Maghana almaarufu Oga Obinna amemshauri mwanamuziki Willy Paul kurejea katika uimbaji wa nyimbo za injili.

Kwenye ujumbe wake aliouchapisha kwenye mtandao wa Instagram, Obinna alisema kuwa nafasi yake Wilson Radido almaarufu Willy Paul bado ipo kwenye sekta wa nyimbo za injili.

Isitoshe, Obinna aliwaomba waimbaji wa nyimbo za kumsifu Mungu, Linet Munyali almaarufu Size 8 na Gloria Muliro kumshika mkono na hata kumuombea aliyekuwa mmoja wao, Willy Paul.

“Ninasubiria siku ambayo Willy Paul atarejea kuimba nyimbo za injili. Nafasi yake bado ipo hata baada ya miaka hii yote,” akaandika huku akionyesha nyimbo alizoimba kitambo mwimbaji huyo.

Hata hivyo, akizungumza kwenye mahojiano miaka iliyopita, Willy Paul alisema kuwa aliondokea sekta hiyo baada ya wasanii wengine kumharibia kazi na kutamani sana afeli kwenye muziki.

Kulingana naye, kuondoka kwenye ulingo wa uimbaji wa nyimbo hizo hakumaanishi kuwa Mungu hambariki kupitia nyimbo anazoimba sasa hivi.

“Kabla nibadilishe njia, nilikuwa napitia changamoto nyingi kwenye sekta ya uimbaji wa nyimbo za injili. Sitaki kuwataja majina lakini watu waliniendea kinyume na kulalamikia muziki wangu ulipochezwa kwenye stesheni kadhaa za redio. Kulikuwa na wakati nilikuwa tu natengemea mapato ya muziki ili niyakimu mahitaji ya mamangu na yangu lakini watu hao hawakujali,” akasema.

Akiongezea, Willy Paul alisema, “Wasanii na DJ walikuwa wakisema kuwa nyimbo zangu si za injili. Ubaguzi na mapendeleo…nilikuwa msanii bora lakini hawa watu hawakuwa wanaona ninachofanya ama walichagua kupuzilia.”

Kupitia changamoto hizo, Willy Paul anasema kuwa aliugua ugonjwa wa msongo wa mawazo na kuna nyakati alikosa pesa za kulipia mahitaji yake.

  • Tags

You can share this post!

Huenda walioliwa pesa za SMS wakisaka majibu ya KCPE...

Afisa asimulia kisa cha kushangaza kuhusu...

T L