• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:05 PM
Afisa asimulia kisa cha kushangaza kuhusu ‘alivyoganda’ na mwanamke ndani ya lojing’i kwa saa 10

Afisa asimulia kisa cha kushangaza kuhusu ‘alivyoganda’ na mwanamke ndani ya lojing’i kwa saa 10

NA MWANGI MUIRURI

Baada ya afisa wa polisi wa kiwango cha Konstebo kukwama kwa saa 10 akiwa kwenye mchezo wa huba na kahaba mmoja mjini Othaya usiku wa kuamkia Jumamosi, alihadithia Taifa Leo Dijitali kuhusu masaibu hayo ya kuogofya.

Swali: Tufahamishe jina lako.

Jibu: Singetaka kujianika zaidi lakini cha kujua ni kwamba mimi ni afisa wa polisi kwa sasa nikihudumu katika Kaunti ndogo ya Mathioya, Kaunti ya Murang’a kituo kikiwa ni cha Kiria-ini.

Swali: Ikawa namna gani bunduki yako ikakwama katika vita vya kurushana roho na kahaba?

Jibu: Ni balaa tupu. Sijawahi kuingiwa na taharuki kama iliyonikumba. Nishawahi kujipata katika urushaniaji wa risasi na wezi wa mifugo katika Baringo mwaka wa 2018 lakini haikuwa na uoga kama huu wangu ndani ya lojing’i.

Swali: Ilikuwa namna gani ukakwama?

Jibu: Haikuwa hata na ilani. Mimi niliingia katika danguro hiyo mwendo wa saa tano usiku. Nikapatana na mwanamke mmoja na baada ya kuongea kidogo tukaafikiana nilale katika chumba chake cha biashara kwa gharama ya Sh1,000. Nilimlipa kupitia simu na tukaingia chumbani.

Swali: Halafu?

Jibu: Nilikuwa nikihisi wasiwasi uliofanya bendera ichelewe kupepea. Ni kama nilikuwa nikipewa onyo na jembe langu niache kukimbizana na balaa lakini sikutilia maanani tahadhari hiyo. Mwendo wa saa nane hivi nilihisi jembe langu limejiandaa kushiriki kilimo na ndipo tukageukania na mwenzangu na hatimaye ngoma ikaanza.

Swali: Ngoma ikaanza?

Jibu: Ndio. Nilijitosa kisimani nikiwa wima lakini nikahisi ni kama nimevutwa ndani kwa utaratibu fulani usio na fujo. Nikafikiria ni kubanwa na kiungo na nikajiandaa kutoka ndio nipige mbizi tena…lakini wapi. Nilikwama.

Swali: Ukakwama kivipi?

Jibu: Sitoki, siingii, sijisikii niko wapi ndani ya kisima. Yaani niko tu lakini ni kama sipo.

Swali: Sasa nyote wawili mkagundua kuna shida?

Jibu: Ndio. Mwanamke aliniambia kwamba alikuwa anahisi uchungu. Mimi nilikuwa nahisi joto tu. Tulijaribu kupaka mafuta, mate na maji ndio tuachane lakini haikusaidia kitu. Mimi nilikumbuka kisa cha afisa mwenzangu aliyekuwa amekwama hivyo tu mjini Kenol na nikajua hii ilikuwa siku yangu. Cha kunitia moyo kilikuwa ufahamu kwamba mwenzangu aliishia kuokolewa hivyo basi kunipa matumaini kwamba hali yangu ingeishia tu kutatuliwa.

Swali: Kwa wakati huu wote sasa mlikuwa mnaongea kuhusu nini?

Jibu: Ilifika mahali kitu saa 12 asubuhi tukapoteza sauti. Tulikuwa tumejaribu mbinu zote za kujinasua bila matokeo ya afueni. Sasa ikawa tunatoa jasho huku maumivu yakimzidi mwanamke nami joto likipita lile la COVID-19. Kimoyomoyo nilianza kuomba sasa afueni ije haraka ndio niondoke kwa hayo masaibu.

Swali: Afueni ilikuja saa ngapi?

Jibu: Mwendo wa saa tatu asubuhi ndio mlango wa tulipokuwa ulivunjwa. Katika harakati za kusaka afueni tuliishia kuanguka chini. Kuna mwanamke alikaa kuelewana na huyu tuliyekuwa tumekwamiliana na alichukua simu na akapigia mtu fulani. Nilisikia akisema kwamba bibi yako amekwama na mwanamume hapa Othaya…hatimaye mwendo wa saa nne na nusu kukaingia watu watatu. Bawabu, mwanamume na mwanamke.

Swali: Ikawa namna gani?

Jibu: Nilijipata sauti imenirejelea. Nilijipata tu nikiomba msamaha bila hata kujua ni kwa nani. Nilisema nilikuwa tayari kulipa fidia…nilijua kwamba mambo yangeishia kuwa fidia kwa kuwa yule afisa mwenzangu Kenol alidaiwa Sh15,000.

Swali: Mambo yaliishia aje?

Jibu: Tuliinuliwa tukiwa pamoja tukarudishwa kwa kitanda. Bawabu na wengine wakakaa kando…tukabaki mimi na mshirika wangu kwa kukwama…halafu mzee fulani aliyesema ndiye mume wa kahaba wangu na mwanamke aliyesema ni mganga. Nilihesabiwa gharama na ikawa Sh13,000. Nilisema nipewe simu yangu na nikatuma pesa hizo.

Swali: Halafu?

Jibu: Mganga aliniagiza nilale sawasawa juu ya mwanamke wangu…nikaagizwa nifunge macho. Nikashtukia nimepigwa kofi kubwa kwa makalio na katika ile hali ya kujitikisa kwa uchungu wa pigo hilo, nikashtukia nimekwamuliwa…sijui vile nilivaa nguo zangu na nikaondoka mahali hapo.

Swali: Sasa utalalamika rasmi ili kisa hicho kichunguzwe?

Jibu: Nilalamike namna gani? Kwani nilikuwa nimetekwa nyara? Si ni mimi niliingia mahali hapo kutafuta raha iliyoishia kuwa karaha?

Swali: Utashiriki ngono ya biashara tena?

Jibu: Hapo sijajua kwa uhakika. Unajua nimekuwa nikinunua huduma hizo kwa muda lakini hii ikaishia kuwa bahati mbaya. Nikiwa na miaka 37, nafikiria nitaoa sasa. Lakini nitajipiga msasa kwanza na nipate mwelekeo muafaka wa kunisukuma mbele.

[email protected]

  • Tags

You can share this post!

Oga Obinna: Namuombea Willy Paul arudi kwa Yesu, muziki wa...

Ruto afufua makato ya nyumba, mara hii akiendea watu wa...

T L