• Nairobi
  • Last Updated April 15th, 2024 2:58 PM
Pasta Ng’ang’a awataka wanawake waachane na Facebook isipokuwa wakihubiri Neno

Pasta Ng’ang’a awataka wanawake waachane na Facebook isipokuwa wakihubiri Neno

NA MERCY KOSKEI

MCHUNGAJI tata wa Kanisa la Neno James Maina Ng’ang’a amewaacha wengi vinywa wazi baada ya kukataza wanawake walioolewa kujiunga na mtandao wa Facebook.

Katika video iliyosambazwa mtandaoni, mhubiri huyo anasikika akisema wanawake kama hao wanapaswa kujiunga na jukwaa hilo ikiwa tu wanahubiri Neno la Mungu au wanafanya biashara.

Pasta Ng’ang’a anasikika akiwakataza wanawake kuposti picha zao mitandaoni, akidai kuwa kufanya hivyo kunachangia waume wao kushtuka na kupoteza maisha wakiona namna watu wengi wanavyowatamani wake wao.

“Tafadhali kama wewe ni mke wa mtu, usiingie kwa Facebook isipokuwa kama unahubiri ama kuna biashara unafanya. Kujianikaanika kwa Facebook siku hizi utaua mume wako,” anasikika akisema.

Ng’ang’a aliendelea kuzungumzia uhusiano wa kiroho akisema hivyo ndivyo shetani anavyofanya kazi nyakati hizi.

“Mwanamume anapomwangalia mwanamke kwa kumtamani, tayari amelala naye na hii inamaanisha kwamba ikiwa unavaa kwa njia ya uchochezi na wanaume 1,000 wanatamani kulala nawe… roho yako itaishiwa,” anaongeza.

Haya yanajiri baada ya pasta huyo kutoa onyo kali kwa waumini wake waliofuzu kwa Digrii.

Pasta huyo aliwataka walio na shahada hiyo ya masomo kuacha kuhudhuria kanisa lake, endapo hawatakubali kuongozwa naye licha ya kutokuwa na Digrii.

Kwenye video iliyochapishwa mitandaoni, Ng’ang’a, anaskika akirusha maneno na matamshi mazito kuhusu washirika wenye Digrii.

“Wenye shahada msije ninapohubiri, nendeni kwenye makanisa yenu mnayohudhuria ibada fupi za dakika mbili, hamuwezi kutawala mambo ya kiroho. Hao wasomi tuheshimiane, Daudi hakujifunza na hata manabii aliowapaka hawakujifunza,” alisema.

Ng’ang’a pia alishutumu watu waliosoma kwa kuumiza ulimwengu, haswa kuhusu masuala kama vile ushoga.

  • Tags

You can share this post!

Omanyala atema kocha Ayiemba na kuajiri kocha Kimani

Afisa wa DCI azuiliwa akidaiwa kupora simu ya mwanamke...

T L