• Nairobi
  • Last Updated February 25th, 2024 10:30 AM
Zuchu aweka ua kulinda ngome ya penzi lake

Zuchu aweka ua kulinda ngome ya penzi lake

NA FRIDAH OKACHI

MWANAMUZIKI Zuhura Othman Soud almaarufu ‘Zuchu’ ameibua tetesi za kuwepo kwa mvutano kati yake na wapenzi wa zamani wa staa na bosi wake Naseeb Abdul almaarufu Diamond Platnumz.

Hii ni baada ya Zuchu kupitia chapisho la Instagram, kutishia kumshikisha adabu yeyote atakayeingilia na kujaribu kuvuruga penzi lao (yeye na Diamond).

Katika ujumbe aliochapisha, Zuchu amemzushia mlengwa wa ujumbe huo huku akiapa hatakubali nafasi yake kuchukuliwa. Pia, Zuchu alimfananisha mgeni huyo na nzi ambaye amekuwa mzuri anazunguka kwa uhuru.

“Kuna nzi kaingia chumbani kwangu yani kashakua huru mpaka anaruka ruka bila wasi wasi. Nikimkamata atahadithia wenzake spendi nzi,” alichapisha Zuchu.

Ujumbe huo ambao haukumtataja ex yeyote wa staa wa Bongo moja kwa moja, ulifanya mashabiki kukisia ulielekezwa kwa Mkenya Tanasha Donna. Mtoto wa Diamond na Tanasha Donna anasomea nchini Tanzania katika shule moja ya kifahari.

Kinachoshangaza masahabiki wengi ni jinsi ambavyo mwanamuziki wa Kenya, Tanasha Donna ameonekana akitumia muda mwingi na familia ya Diamond, na hivi karibuni alionekana akiendesha gari jupe aina ya Land Cruiser alilozawadiwa na Diamond miaka michache iliyopita.

Yapo madai kwamba Tanasha Donna amepangishiwa nyumba na Diamond aliyemshauri kuishi nchini Tanzania.

Safu hii imejaribu kuthibitisha madai hayo lakini Tanasha Donna hakujibu simu.

Katika video ya Instagram kwenye Wasafi TV, Tanasha Donna alikuwa kwenye mazungumzo ya kirafiki na sajili mpya wa lebo ya Wasafi (WCB), D Voice, akitoa pongezi kwa mafanikio yake ya hivi majuzi.

WCB inamilikiwa na Diamond.

Tanasha Donna alielezea kufurahia kipindi chake cha hivi majuzi.

“Nilikuona na nilifurahia kipindi cha jana (siku hiyo) nilipokuwa nakitazama runinga,” Tanasha Donna alimuambia D Voice.

Hayo kando, wiki jana Zuchu na Diamond walikuwa nchini Afrika Kusini kurekodi kipindi kitakachopeperushwa kwa Young, Famous and African.

Hata hivyo mamake Zuchu, malkia wa Taarab nchini Tanzania Bi Khadija Kopa aliwahi kukana kuwepo kwa uhusiano wa kimapenzi baina ya wawili hao, kwa kile alitaja hatapokea mahari kutoka kwa staa huyo.

  • Tags

You can share this post!

Sasa madiwani watishia kumbandua Naibu Gavana wa Trans Nzoia

Taasisi 70 za kozi za kiufundi kupigwa jeki ya Sh8.8 bilioni

T L