• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 8:50 AM
BORESHA AFYA: Mlo bora kwa afya ya akili

BORESHA AFYA: Mlo bora kwa afya ya akili

NA PAULINE ONGAJI

CHAKULA unachokula kina umuhimu sio tu kwa mwili, bali pia kwa afya ya akili.

Wataalamu wanasema kwamba kuna baadhi ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kuimarisha akili kama vile;

•Mimea: Utafiti wa mwaka wa 2020 uliochapishwa kwenye jarida la Clinical Nutrition, ulionyesha kwamba lishe inayohusisha mimea ina viwango vya chini vya msongo wa mawazo, wasiwasi na matatizo ya kisaikolojia miongoni mwa wanawake.

•Vyakula vya baharini: Vyakula kama samaki aina ya samoni vina manufaa mengi kutokana na viwango vya juu vya kemikali za mafuta ya omega-3. Watafiti wametambua ulaji wa vyakula vya viwango vya juu vya kemikali za mafuta ya omega-3 huzuia msongo wa akili.

•Nafaka ambazo hazijakobolewa: Nafaka hizi husaidia kukabiliana na msongo wa mawazo. Aidha, utafiti uliochapishwa hivi majuzi ulionyesha kwamba wanawake wanaokula viwango wastani vya nafaka hizi huwa na uwezekano mdogo wa kukumbwa na matatizo ya wasiwasi.

•Kokwa: Utafiti unaonyesha kwamba watu wanaokula kokwa kwa wingi wana uwezekano mdogo wa kukumbwa na msongo wa mawazo wakilinganishwa na wasiokula chakula hiki. Mbali na hayo, kokwa zina viwango vya juu vya mafuta ambayo hayajakolezwa (unsaturated fat), na utafiti unaonyesha kwamba watu wanaotumia mafuta ya aina hii wana uwezekano mdogo wa kusumbuliwa na matatizo ya wasiwasi.

•Matunda madogo: Watu wanaokula matunda madogo kwa wingi wana uwezekano mkubwa wa kuwa na afya njema ya kiakili.Kwa mfano, matunda ya ‘wild blueberries’ yana manufaa kwani yana viwango vya juu vya madini ya manganizi ambayo ni muhimu katika kudumisha afya ya akili.

  • Tags

You can share this post!

JIJUE DADA: Kukabili tatizo la upele na mwasho kwenye...

DKT FLO: Je, uzito kifuani huletwa na nini?

T L