• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
DKT FLO: Je, uzito kifuani huletwa na nini?

DKT FLO: Je, uzito kifuani huletwa na nini?

Nini kinachosababisha uzito kwenye kifua?

Kris, Mombasa

Mpendwa Kris,

Hii ni mojawapo ya ishara kuu za mshtuko wa moyo na hivyo unashauriwa kutafuta matibabu kila unaposhuhudia dalili hii.

Nini kinachosababisha hali hii?

Japo kwa wingi mshtuko wa moyo husababisha ishara hii, kuna vichocheo vingine ambavyo sio hatari kwa maisha. Mashambulizi ya uoga yaani ‘Panic attack’ pia huwa na ishara hii na wakati mwingi hudhaniwa kuwa mshtuko wa moyo.

•Angina ni maradhi mengine ya moyo ambayo husababisha mgonjwa kuhisi uzito kwenye kifua.

•Gastroesophageal reflux disease (GERD) pia ni mojawapo ya hali zinazoambatana na ishara ya uzito katika sehemu ya kifua. Hali hii hutokea asidi na chakula tumboni zinaporejea kwenye umio. Ili kuzuia hali hii unashauriwa kupumzika baada ya kula.

•Maradhi ya pumu humsababisha mgonjwa kushindwa kupumua na hivyo kumpelekea kuhisi uzito kwenye kifua.

•Jeraha kwenye mbavu.

•Aortic aneurysm ni hali ambayo hutokea wakati ukuta wa mshipa wa aota unapodhoofika na kuvimba na kuhatarisha maisha ya mgonjwa.

Ishara

Hisia za mkazo kifuani zikiandamana na maumivu ya mgongo, mikono, taya, shingo na mabega.

Uchovu, wasiwasi, kisunzi, kichefuchefu, kutokwa na jasho jingi na kushindwa kupumua.

Mojawapo ya njia za kukabiliana na hali hii ni kubadili mtindo wa kimaisha kama vile kutovuta sigara, kuchunguza msukumo wa damu kila mara, kuchunguza kiwango cha sukari katika damu kila mara, kufanyiwa uchunguzi wa ‘cholesterol’ mwilini angalau mara moja kwa mwaka, kufanya mazoezi kila wakati, kupunguza mawazo, kudumisha uzani unaofaa na kuzingatia lishe bora.

You can share this post!

BORESHA AFYA: Mlo bora kwa afya ya akili

Kocha Mwalala apigwa kalamu Homeboyz FC

T L