• Nairobi
  • Last Updated December 5th, 2023 8:55 PM
Chagua vinywaji hivi badala ya kahawa kila mara

Chagua vinywaji hivi badala ya kahawa kila mara

NA MARGARET MAINA

[email protected]

INGAWA kahawa ina baadhi ya manufaa ya kuvutia, kuna njia mbadala na hakuna krimu au sukari inayohitajika.

Unaamshwa na saa ya kengele, unajikokota kutoka kitandani, unatengeneza kahawa, na unaruka kutoka kwa hali ya ulegevu na kusisimka.

Ingawa kahawa huleta athari chanya na manufaa ya kuvutia (ikiwa ni pamoja na kuongeza utambuzi, kuzuia unyogovu, kutaja tu manufaa machache) inaweza kuwa na athari hasi.

Hata hivyo, baadhi ya vinaweza vinaweza kutumika kama mbadala kwa kafeini. Isitoshe, vinywaji hivyo vina nishati ya asili bila sukari mbaya.

Sharubati ya machungwa

Glasi ya sharubati ya machungwa asubuhi inaweza kuongeza nishati ya ubongo kwa siku nzima.

Maji ya nazi

Maji ya nazi kiasili yana kalori chache na yana kiwango kikubwa cha elektroliti za kurejesha maji mwilini na madini kama sodiamu na potasiamu.

Usawa wa elektroliti husaidia kupigana na uchovu na kupambana na udhaifu wa misuli na tumbo, ambayo pia hufanya kuwa kinywaji kinachotafutwa sana cha kujipatia nafuu baada ya mazoezi.

Juisi ya komamanga

Juisi ya komamanga ni mojawapo ya dawa mbadala za kafeini zinazofaa zaidi. Inaweza kuboresha utendaji wa mazoezi kwa kuboresha mzunguko wa damu na mtiririko pamoja na kuimarisha misuli.

Mnanaa

Harufu na ladha ya mnanaa inaweza kufanya mtumiaji kuibua kumbukumbu nzuri na kuongeza umakini na usikivu.

Kombucha

Kombucha kimsingi ni chai tamu iliyochachushwa na chachu. Vitamini B iliyomo ni muhimu katika utengenezaji wa nishati, kwani husaidia kubadilisha vyakula tunavyokula kuwa nishati inayoweza kutumika mwilini.

Kuanza siku na kimojawa cha vinywaji vyenye afya zaidi si tu kunaboresha uzalishaji wa nishati, lakini pia husaidia kuboresha afya ya utumbo na kuimarisha mfumo wa kinga.

Vitamini B

Kwa mshikamano unaojulikana kama B tata, vitamini B 12 ni muhimu kwa kusaidia mifanyiko ya kimetaboliki yenye afya na kutoa nishati ya siku nzima.

Pata vitamini B kupitia vyanzo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mkate wa nafaka nzima na nafaka, chachu, kwinoa, shayiri, kuku, nyama ya viungo, tuna, maziwa, mtindi, jibini, maharagwe, dengu, mbaazi, mboga za majani, viazi, uyoga, ndizi, machungwa na kahawa.

  • Tags

You can share this post!

Manufaa ya mafuta ya mbegu nyeusi ambazo kwa jina la...

Mkenya Evans Chebet ahifadhi ubingwa wa Boston Marathon

T L