• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 3:08 PM
Manufaa ya mafuta ya mbegu nyeusi ambazo kwa jina la kisayansi ni Nigella sativa

Manufaa ya mafuta ya mbegu nyeusi ambazo kwa jina la kisayansi ni Nigella sativa

NA MARGARET MAINA

[email protected]

MAFUTA ya mbegu nyeusi, ambazo zinajulikana kisayansi kama Nigella sativa, yana bioactive ambayo ni muhimu kwa afya ya ngozi na nywele, husaidia kupunguza uvimbe, na husaidia vile vile kupunguza uzito.

Katika sehemu nyingi za ulimwengu, mbegu nyeusi hutumiwa kama dawa ya kitamaduni ya ugonjwa wa sukari na shinikizo la damu. Katika baadhi ya tafiti ndogo, virutubisho vilivyotengenezwa kutokana na mbegu nyeusi vimeonyesha viwango vya chini vya lehemu na mafuta ya damu.

Mafuta ya mbegu nyeusi ni kiungo cha mitishamba kinachotokana na mmea wa Nigella sativa, ambao asili yake ni Ulaya Mashariki na Magharibi mwa bara Asia.

Aidha, mbegu nyeusi hujulikana kwa sifa zake za nguvu za dawa ya kiasili ambayo watu hutumia kutibu magonjwa anuwai, pamoja na:

  • maumivu ya kichwa
  • maumivu ya mgongo
  • shinikizo la damu
  • maambukizi
  • kuvimba

Pia mbegu hizi zina manufaa mengine ya kiafya na katika urembo.

Kukuza afya ya usagaji chakula

Mojawapo ya matumizi yanayotambulika zaidi ya mafuta ya mbegu nyeusi ni katika uimarishaji wa mfumo mzima wa usagaji chakula, kwani hutumiwa sana kutibu tumbo, kukabili matatizo ya gesi, kuhara, kuvimbiwa, na ugonjwa wa bawasiri.

Kudhibiti sukari ya damu

Mafuta ya mbegu nyeusi yanaweza kudhibiti sukari ya damu.

Kupunguza chunusi

Mafuta ya mbegu nyeusi yanaweza kuwa na manufaa kwa ngozi, kama vile kukabili chunusi.

Uponyaji wa jeraha

Mafuta ya mbegu nyeusi yana ‘kiwanja’ ambacho kina uwezo wa kuchochea ukuaji wa tishu na kukuza uponyaji wa jeraha.

Mafuta haya yanaweza kusaidia kutibu majeraha ya kuungua, kukatwa na majeraha ya kisukari. Ni mafuta muhimu ya kuzuia ukuaji au ueneaji wa bakteria.

Udhibiti wa sukari ya damu

Mafuta ya mbegu nyeusi yanaweza kuwa na manufaa kwa kuimarisha viwango vya sukari ya damu. Yanaweza kusaidia kuboresha viwango vya insulini na viwango vya sukari ya damu wakati wa kufunga na baada ya chakula.

Mbegu nyeusi ina ufanisi katika kupunguza kasi ya sukari ya damu na kupunguza viwango vya hemoglobini A1C, kipimo cha udhibiti wa sukari ya damu kwa muda mrefu.

Mafuta haya huwa ni ya bei nafuu na yanapatikana kwa wingi katika maduka mengi ya dawa na maduka ya lishe ya afya.

  • Tags

You can share this post!

Tabia na hali zinazohusishwa na ugonjwa wa mishipa ya moyo...

Chagua vinywaji hivi badala ya kahawa kila mara

T L