• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 5:50 AM
Chakula kinachoweza kusaidia kuimarisha nywele

Chakula kinachoweza kusaidia kuimarisha nywele

NA MARGARET MAINA

[email protected]

KUNA mengi ambayo hufanya nywele zako ziwe zenye afya.

Kwa mfano, usafi mzuri, kukata nywele kwa wakati na bidhaa za huduma za nywele.

Mbali na haya, chakula pia huchangia katika kufanya nywele zako kuwa na nguvu, zenye kupendeza na zenye afya.

Chakula sahihi husaidia kuweka nywele zenye afya kutoka ndani. Ili kukuza nywele zako na kufanya nywele zako ziwe na afya, unahitaji protini. Kama vile mwili wetu unahitaji protini kufanya kazi vizuri, vivyo hivyo nywele zetu zinahitaji protini kwa lishe.

Haijalishi ubora wa nywele zako ni nini, kula protini ya kutosha kutazifanya kuwa na nguvu.

Mchicha

Mchicha ni aina ya mboga za majani zenye virutubisho vingi. Aidha, mchicha huwa na Vitamini A, vitamini K na vitamini C ambazo husaidia kulinda na kudumisha utando wa seli za mizizi za nywele.

Mbegu za Chia

Mbegu za chia. PICHA | MARGARET MAINA

Unaweza kuziongeza kwa nafaka, puddings, smoothies, saladi na zaidi.

Dengu

Dengu ni chanzo kikubwa cha protini ya mboga, nyuzinyuzi, fosforasi na asidi ya folic. Virutubisho hivi vyote hufanya kazi ya kusambaza oksijeni kwenye ngozi ya kichwa na kuchochea ukuaji wa nywele. Protini katika dengu ni muhimu kwa ukuaji wa nywele na afya ya nywele kwa ujumla.

Mayai

Mayai ni chanzo kikubwa cha protini na biotini, virutubisho viwili ambavyo ni muhimu sana kwa ukuaji wa nywele. Kula protini ya kutosha ni muhimu kwa ukuaji wa nywele kwa sababu mizizi ya nywele hutengenezwa kwa protini.

  • Tags

You can share this post!

Faida za kuwa na kijishamba cha mboga nyumbani

MAPISHI KIKWETU: Mchuzi wa njegere na viazi mbatata

T L