• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 6:50 AM
MAPISHI KIKWETU: Mchuzi wa njegere na viazi mbatata

MAPISHI KIKWETU: Mchuzi wa njegere na viazi mbatata

NA MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 20

Muda wa mapishi: Dakika 40

Walaji: 2

Vinavyohitajika

  • viazi 2 kubwa
  • karoti 1 kubwa
  • vitunguu maji vyekundu 2 vilivyokatwa
  • punje 4 za kitunguu saumu
  • nyanya 1 iliyokatwa
  • vijiko 1 ½ vya nyanya ya kopo
  • kijiko ½ cha manjano
  • vikombe 2 vya njgere zilizopikwa
  • kijiko ½  cha bizari nyembamba
  • kijiko 1 cha poda ya curry
  • kijiko 1 cha kitunguu ya poda
  • chumvi na pilipili
  • majani ya giligilani

Maelekezo

Kabla ya kupika, kila kitu kinapaswa kutayarishwa. Chonga viazi na uvikate vipande vipande.

Kwenye sufuria yako, weka mafuta, chumvi na pilipili, kisha ongezea vitunguu vyekundu na vitunguu saumu halafu kaanga hadi viwe na harufu nzuri na vilainike.

Ongeza nyanya ya kawaida, nyanya ya kopo na viungo vingine na upike hivi hadi ladha ziwe pamoja na mchanganyiko uwe mzuri na mzito.

Ongeza manjano. Hii ina faida nyingi za kiafya. Vile vile huongeza rangi hiyo ya manjano na kufanya chakula chako kionekane kizuri na cha kusisimua.

Nyanya zinahitajika kupikika kwa muda. Mchuzi unapaswa kuwa mzuri na mzito ili kitoweo chako kiwe kizito pia. Ukipika kitoweo na kila mara unapata nyanya zinazoelea kama jeli kwenye sahani yako, hayo ni matokeo ya kuharakisha kupika. Kuwa na subira kidogo zaidi na utakuwa na matokeo mazuri kila wakati.

Ongeza kwenye viazi vyako karoti na maji kidogo / hisa ili kuwezesha kupikia viazi.

Ikiwa una nyama iliyopikwa, unaweza kuiongeza katika hatua hii.

Kwa sababu viazi ushavikatakata, vitaiva haraka. Muda utatofautiana kulingana na saizi ya viazi vyako.

Acha chakula hiki kichemke kwa muda wa dakika 15 na mara tu viazi vimekwisha iva, ongezea njegere zilizopikwa.

Ongezea majani ya giligiani kisha epua. Pakua na ufurahie.

  • Tags

You can share this post!

Chakula kinachoweza kusaidia kuimarisha nywele

MAPISHI KIKWETU: Matoke na nyama ya mbuzi iliyokaangwa

T L