• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 8:55 AM
Chukua tahadhari dhidi ya vyakula hivi ikiwa una tatizo la mawe kwenye kibofu

Chukua tahadhari dhidi ya vyakula hivi ikiwa una tatizo la mawe kwenye kibofu

NA MARGARET MAINA

[email protected]

SASA kwa kuwa tunajua ni vyakula gani tunapaswa kujumuisha katika lishe yetu kwa kibofu chenye afya, hebu tuangalie baadhi ambavyo tunapaswa kuepuka.

Mkate na wanga

Baadhi ya kabohaidreti ambazo unahitaji kujiepusha nazo ni:-

  • vyakula vya kuoka vilivyochakatwa
  • chakula kilichoongezwa sukari, tamutamu na chokoleti
  • unga mweupe na nafaka iliyosafishwa

Mafuta

Nyongo inayozalishwa kwenye kibofu husaidia kuyeyusha mafuta. Hata hivyo, ni vigumu kuvunja mafuta yaliyojaa, ambayo yanaweza kuongeza mkazo kwenye kibofu. Baadhi ya vyanzo vikubwa vya mafuta haya yasiyofaa ni:-

  • nyama iliyosindikwa na nyama nyekundu
  • bidhaa za maziwa (usijumuishe zile zenye mafuta kidogo)
  • vyakula vilivyosindikwa na kukaangwa
  • chokoleti na aiskrimu

Vidokezo kadhaa vya kupona haraka baada ya kuondolewa kwa kibofu

Uondoaji wa kibofu cha nyongo hauna madhara yoyote mabaya kwenye mfumo wa utumbo wa mwili.

Walakini, mifumo yao itachukua muda kurekebishika, wakati ambao lazima wafanye mabadiliko fulani ya lishe ili kuendana na hali ya mwili. Baadhi ya vidokezo vya kawaida ni pamoja na:-

  • kula milo midogo lakini ya mara kwa mara
  • punguza ulaji wa mafuta na utumie vyakula mbadala vyenye mafuta kidogo au kiasi
  • epuka kafeini; vyakula vyenye viungo na chochote ambacho kinaweza kusumbua mfumo wako wa usagaji chakula
  • kula vyakula vyepesi vilivyo rahisi kusagika
  • daima hakikisha unashauriana na daktari wako ikiwa unakabiliwa na kichefuchefu na maumivu
  • Tags

You can share this post!

Tiba za nyumbani kwa maumivu ya kisigino

MAPISHI KIKWETU: Wali wa kukaangwa na kuku

T L