• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 7:12 PM
MAPISHI KIKWETU: Wali wa kukaangwa na kuku

MAPISHI KIKWETU: Wali wa kukaangwa na kuku

NA MARGARET MAINA

[email protected]

WALI wa kukaangwa na kuku ni mlo unaopendwa sana China na bara Asia kwa ujumla.

Mlo huu ulianza kama njia ya kutumia mabaki ya wali kwa kuongeza mafuta na mchuzi wa soya na mboga mboga na nyama na kuupa wali ladha.

Muda wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa mapishi: Dakika 5

Walaji: 2

Vinavyohitajika

vijiko 3 vya mafuta ya mzeituni

kuku kilo ½ bila mifupa

chumvi

pilipili nyeusi

vijiko 2 vya ufuta

vitunguu maji 2, vilivyokatwakatwa

karoti 2, kwangua na kata vipande vipande

punje 3 kitunguu saumu, kusaga

kijiko ½ tangawizi ya kusaga

vikombe 2 vya mchele mweupe uliopikwa (ikiwezekana uliobaki)

kikombe ½  mbaazi

mayai 4, yaliyopigwa

mchuzi wa soya

vitunguu 2 vya kijani, vikate vipande vyembamba

Maelekezo

Kwenye kikaangio kwa moto wa kati, pasha moto mafuta ya mzeituni.

Tumbukiza vipande vya kuku na chumvi na pilipili viive pande zote mbili, kisha uongeze kwenye sufuria, na upike hadi iwe na rangi ya dhahabu na isiungue; dakika nane kila upande.

Ondoa kwenye sufuria na uruhusu nyama hii ipoe kwa dakika tano, kisha ukate vipande vipande.

Katika kikaangio ulichokitumia awali, pasha kijiko kimoja cha mafuta ya ufuta.

Ongeza kitunguu na karoti na upike hadi vilainike kwa dakika tano. Ongeza kitunguu saumu na tangawizi na upike hadi viwe na harufu nzuri. Utatumia dakika moja zaidi.

Koroga wali na mbaazi na upike hadi wali upate joto baada ya dakika mbili hivi.

Sukuma wali kwa upande mmoja wa sufuria na uongeze kijiko kilichobaki cha mafuta ya ufuta kwa upande mwingine.

Ongeza mayai na koroga hadi yaive kabisa, kisha kunja mayai kwenye wali. Ongeza kuku nyuma kwenye sufuria na mchuzi wa soya na vitunguu kijani na koroga ili kuchanganya.

  • Tags

You can share this post!

Chukua tahadhari dhidi ya vyakula hivi ikiwa una tatizo la...

Kilio Seneti wahasiriwa wakisimulia masaibu yao mikononi...

T L