• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 3:16 PM
Faida ya korosho kwa mwili wa binadamu

Faida ya korosho kwa mwili wa binadamu

Na MARGARET MAINA

[email protected]

KOROSHO ni muhimu sana katika mwili wa binadamu ijapokuwa hutumika kwa nadra sana kutokana na ugumu wa upatikanaji wake na bei ghali.

Kisayansi inashauriwa kutumia korosho kiasi, nafaka hii ina virutubisho muhimu na adimu. Imebainisha kuwa mtu anayetumia korosho hufaidika kwa kuongeza vitu vifuatavyo mwilini.

Korosho ina wanga, vitamini, kalsiamu, mbali na madini hayo ina umiliki mkubwa wa madini ya Zinki, Magnesium, Potassium, Copper, na Asidi ya Folik.

Hivyo katika mwili wa binadamu korosho husaidia mambo yafuatayo:

Inasaidia kunyonya mafuta katika mwili wa binadamu hivyo huulinda mwili dhidi ya magonjwa ya moyo na kuusaidia moyo kuwa wenye afya njema.

Huepusha ugonjwa wa Anemia na magonjwa mengine ya damu, kula korosho mara kwa mara husaidia mwili kuwa na madini ya chuma ambapo ugonjwa wa Anemia hutokana na upungufu wa madini ya chuma hivyo ulaji wa korosho hukinga mwili na magonjwa ya damu ikiwemo Anemia.

Korosho husaidia uwezo wa macho kuona kama ilivyo kwa karoti, kutokana na uchafuzi mkubwa wa mazingira macho yapo katika hatari kubwa ya kudhurika, korosho ina miliki kirutubisho kisayansi kinajulikana kama Zea Xanthin ambacho huilinda Retina ya jicho dhidi ya miale na uchafu ambao unaweza kudhuru jicho.

Nzuri kwa kutunza ngozi, kutokana na mafuta yanayomo ndani ya korosho yenye virutubisho na madini kwa kung’arisha ngozi madini hayo ni kama Zinki, Magnesium, Fosfora na chuma lakini pia uwepo wa madini ya selenium ambayo hulinda ngozi dhidi ya magonjwa ya kansa.

Lakini pia kwa wale wenye uhitaji wa kupunguza uzito, kisayansi inashauriwa kutumia kiasi nafaka ya korosho ili kupunguza uzito wa mwili, korosho inamiliki aina tatu za asidi ambazo husaidia mfumo unaoratibu mwili kuvunja vunja mafuta ya ziada.

Pia mtu anayekula korosho ana wakati mzuri wa kufanya nywele zake ziwe na afya nzuri hii ni kutokana na mafuta yanayotokana na korosho.

You can share this post!

Faida za mbegu za maboga

Ruto amhepa Uhuru