• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 9:50 AM
Faida za kiafya kunywa chai ya chamomile

Faida za kiafya kunywa chai ya chamomile

NA MARGARET MAINA

[email protected]

CHAI ya Chamomile imejaa antioxidants. Faida kuu za kiafya za chai ya chamomile zinaweza kujumuisha uwezo wa kudhibiti usingizi, kusaidia usagaji chakula, kuongeza kinga, kulinda ngozi, kupunguza mfadhaiko, na kutuliza maumivu ya hedhi.

Chai ya Chamomile ina ladha ya kupendeza. Inajulikana sana kwa faida zake za kiafya.

Ingawa hutumiwa kuunda kinywaji, chamomile pia hutumiwa katika vidonge na mafuta ya aromatherapy.

Losheni ya chamomile hutumika ili kukabili baadhi ya matatizo mbalimbali ya ngozi.

Kwa undani faida za kunywa chai ya chamomile ni kama vile;

– Inaweza kukufanya upate usingizi

Ukinywa chai ya chamomile unaweza kupata usingizi kwa urahisi. Athari hii haswa ni kwa watu wanaotatizika na kukosa usigizi. Kunywa kikombe cha chai ya chamomile isiyo na kafeini kunaweza kukusaidia kulala haraka na kuamka ukiwa umetuliza akili vya kutosha Inapendekezwa sana kwa akima mama pindi baada ya kujifungua ili kuboresha ubora wa usingizi wao.

– Inaweza kupunguza kuvimba

Ikiwa unasumbuliwa na mwasho wa tumbo, kuanzia uvimbe mdogo hadi dalili za ugonjwa wa matumbo kuwa ni kama yanawaka, chai ya chamomile inaweza ikakufaa pakubwa. Kunywa chai ya chamomile mara kwa mara kunaweza kusaidia kupunguza matatizo kama vile kichefuchefu, mkazo wa misuli, mafua ya tumbo, na ugonjwa wa tumbo.

– Inaweza kukuza afya ya moyo

Chai ya chamomile inaweza kusaidia kupunguza shinikizo la damu na viwango vya lehemu mbaya, na kufanya moyo wako kuwa wenye afya. Chai hii pia inaweza kupunguza matukio ya masuala mbalimbali ya moyo na mishipa.

– Inaweza kuimarisha mfumo wa kinga

Chai ya chamomile inaweza kusaidia kuimarisha mfumo wako wa kinga na kuzuia maambukizo. Michanganyiko mingine iliyopo katika chai ya chamomile inaweza pia kupambana na baridi, mafua na matatizo ya sinus, hatimaye kupunguza msongamano.

– Inaweza kuondoa dhiki na wasiwasi

Mojawapo ya matumizi maarufu ya chai ya chamomile ni kuwa inaleta utulivu mtu akatoka kwa mfadhaiko na wasiwasi. Baada ya siku ndefu kazini, kujituliza kwa kinywaji hiki kunaweza kusaidia kuongeza viwango vya serotonin na melatonin katika mwili wako. Homoni hizi zinaweza kusaidia kuondoa mafadhaiko na wasiwasi. Kunywa chai hii pia kunasaidia kupumzika, inaweza kusaidia kuondoa dalili za kawaida za wasiwasi. Chai ya chamomile pia inaweza kusaidia kupunguza dalili za kunyong’onyea kwa wanawake baada ya kujifungua.

  • Tags

You can share this post!

Ufisadi: Karua atia ahadi yake doa kuu

FIDA yahimiza wapigakura kuchagua wanawake kuongeza idadi...

T L