• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 9:50 AM
Faida za pilipili mboga

Faida za pilipili mboga

Na MARGARET MAINA

[email protected]

PILIPILI mboga sio kitu kigeni kwetu kwa sababu tunaijua na huwa tunaitumia nyumbani.

Wengi wetu tunaitumia kama kiungo cha mboga na wengine hutumia katika kutengeneza kachumbari ili kuleta ladha.

Pilipili mboga sio kali au chungu na hutofautiana katika ukubwa

Hupatikana katika mwonekano wa rangi tofauti tofauti kama vile nyekundu, kijani, urujuani na njano.

Faida za kiafya za pilipili mboga katika mwili wa binadamu

Pilipili mboga huimarisha kinga ya mwili uweze kupambana na magonjwa mbalimbali.

Husaidia kuongeza uwezo wa kuona kwa wale wenye matatizo ya macho. Hivyo ni vyema kutumia kiungo hiki cha chakula ili kuongeza uwezo wa kuona vizuri.

Pilipili mboga husaidia mwili kupambana na magonjwa ya moyo.

Juisi ya pilipili mboga husaidia kuchuja taka mwilini.

Hutibu muwasho wa vidonda vya kooni.

Pilipili mboga. Picha/ Margaret Maina

Pilipili mboga zina vitamini C ambayo husaidia kutibu ugonjwa wa kutokwa damu puani na kuimarisha kinga ya mwili.

Kupunguza mafuta yasiohitajika mwilini hivyo huweza kupunguza uzani.

Kuimarisha mzunguko wa damu mwilini pamoja na kupunguza shinikizo la damu.

Huzuia na kuondoa gesi tumboni kwa mwenye tumbo iliyojaa gesi hii.

Kutokana na kuwa na wingi wa vitamini C, vitamini hii hupigana dhidi ya magonjwa na kujenga kinga imara ya mwili.

Husaidia kwa wenye matatizo katika mfumo wa upumuaji mfano asthma yaani pumu.

Hutibu ugonjwa uitwao baridi yabisi (rheumatism). Huu ni ugonjwa wa kukakamaa sehemu mbalimbali za mwili kama vile mifupa, misuli na viungo vya mwili.

Husafisha ngozi na pia ni lishe nzuri sana.

Husaidia katika mmeng’enyo wa chakula kufanyika vizuri.

  • Tags

You can share this post!

Wito serikali ipige jeki sekta ya juakali

Kampuni za ndege Afrika zakumbatia teknolojia ya paspoti za...