• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 8:46 PM
FASIHI SIMULIZI: Udhaifu wa mbinu za ukusanyaji data

FASIHI SIMULIZI: Udhaifu wa mbinu za ukusanyaji data

JUMA lililopita, tuliangazia umuhimu wa mbinu za ukusanyaji data ya Fasihi Simulizi.

Leo tutajadili udhaifu wa mbinu zizo hizo kwa manufaa ya mtafiti.

MAHOJIANO

Udhaifu

  • Ni mbinu inayohitaji muda mrefu kwani mtafiti na mtafitiwa hutumia wakati mwingi kukutana ana kwa ana.
  • Mhojiwa anaweza kutoa habari za uwongo kwa sababu hawajuani.Kikwazo cha mawasiliano iwapo watafitiwa au jamii lengwa haijui kusoma na kuandika.
  • Ni mbinu ghali kutokana na gharama ya usafiri ikiwa walengwa ni wa mbali.
  • Ufisadi – wahojiwa wakati mwingine huitisha mlungula/hongo kabla ya kukubali kushiriki katika mahojiano.

KUTAZAMA/UTAZAMAJI

Udhaifu

  • Hata kama huhitaji kitendo cha kutazama tu, mawasiliano yaweza kuwa kikwazo iwapo mtafiti hafahamu lugha ya watafitiwa.
  • Ukosefu wa uaminifu humfanya mtafitiwa kukosa kutoa ujumbe wa kweli.
  • Ni ghali kwa sababu mtafiti lazima asafiri hadi nyanjani mwa watafitiwa.

KUREKODI KATIKA KANDA ZA SAUTI/TEPUREKODA/VIDEO/FILAMU

  • Nguvu za umeme zinaweza kukosekana/kutoweka hivyo utafiti kuathiriwa.
  • Vifaa hivi haviwezi kunasa hisia, viziada lugha na uigizaji kwa jumla.
  • Fanani anaweza kuupiga chuku uwasilishaji wake hata kupoteza ujumbe kwa sababu anajua kuwa anarekodiwa.
  • Ni mbinu ghali kwani mtafiti anahitaji kununua kifaa na kumbidi mtafiti kusafiri.

HOJAJI

Udhaifu wa Hojaji

  • Kunaweza kutokea utata wa maswali na hivyo kusababisha majibu yasiyo sahihi.
  • Wasiojua kusoma na kuandika hawatatumia mbinu hii
  • Itakuwa vigumu kupata sifa za uwasilishaji kama vile kiimbo, toni na ishara/viziada lugha.
  • Wahojiwa wanaweza kukataa kuijaza kutokana na mwelekeo hasi dhidi ya hojaji na hivyo kukwamiza utafiti.

Kipkoros Borwo

Alliance Girls High School

  • Tags

You can share this post!

TUSIJE TUKASAHAU: Rais Kenyatta asisahau serikali yake...

Wanasiasa wasukumwa kueleza mipango ya kuinua utalii

T L