• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 12:42 PM
Fuata utaratibu huu kuandaa keki yenye ladha tamu

Fuata utaratibu huu kuandaa keki yenye ladha tamu

Na MARGARET MAINA

[email protected]

KILA siku kuna malalamiko, “keki yangu haijachambuka, ni mbichi ndani na kadhalika.”

Fuata utaratibu huu na utapata matokeo mazuri.

Usipige mchanganyiko wa keki kupita kiasi. Unapofanya hivyo, unaua nguvu ya baking powder na kusababisha keki yako kutoumuka na kubonyea katikati.

Hakikisha baking powder unayotumia unaangalia tarehe yake ya kuharibika na pia isiwe imekaa siku nyingi sana. Nayo pia husababisha keki kutoumuka.

Unapoweka keki ndani ya ovena au hata kama utaoka katika jiko la makaa, usipende kufungua mara kwa mara. Hewa inapotoka nje, keki hubonyea katikati na pia kutoka mbichi kwa ndani.

Unapoweka keki ndani ya ovena au katika jiko la makaa, kuwa mstahamilivu na fungua kwa nadra sana. Na unapofungua, fungua kiasi tu na wala sio unafungua yote kwani hewa ikitoka matokeo ya keki yanakuwa sio mazuri.

Ukitaka kujua keki kama imeiva fungua, kidogo tu na ingiza ncha ya kijiko au kisu ukiona kimetoka safi kabisa bila ya kugandiwa na mchanganyiko wa keki, basi keki iko tayari.

Ukishatoa keki iache na chombo chake ipoe. Ni baada ya kupoa kabisa ndipo unafaa kuanza kuikata. Ukikata ikiwa ingali moto, keki humomonyoka na kupondekapondeka.

Hakikisha kufuata masharti na vipimo vya maelekezo yoyote ya keki utakayotumia kuioka ndipo upate matokeo mazuri.

Sio keki zote lazima ziwe zina baking powder. Zipo namna nyingi za kuoka keki. Ukiona katika vinavyohitajika kuoka keki hakuna baking powder, usishtuke. Katika uokaji, baadhi ya keki katika kuzioka, wapishi hutumia bicarbonate of soda. Vile vile keki yaweza ikaokwa pasi na ngano au mayai.

Zingatia kipimo cha baking powder kinachohitajika kwa sababu ukizidisha, keki yako huchambuka kupita kiasi na kupondekapondeka.

Hakikisha keki imepoa kabisa kabla hujaanza kuipamba kwa icing. Ndio utapata matokeo mazuri. Keki haipambwi ikiwa ingali moto.

Keki inapohitaji siagi isiyokua na chumvi basi tumia siagi isiyokuwa na chumvi.

Pia wengi hulalamika kuwa keki inapasuka kwa juu. Hii ni kwa sababu ya chombo kuwa kidogo na kwa hiyo kubana nafasi ya keki pale inapoumuka na kufanya keki yako kupasuka kwa juu. Hakikisha unakadiria upana wa chombo na mchanganyiko wa keki. Hapo utapata keki inatoka vizuri kabisa juu bila ya kupasuka.

You can share this post!

Wanajeshi wa Ulinzi Stars wakabwa na Stima, Mathare ikipata...

Majaji watano wazima IEBC kupeleka mswada wa BBI kwa kaunti...