• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 3:46 PM
Majaji watano wazima IEBC kupeleka mswada wa BBI kwa kaunti kujadiliwa

Majaji watano wazima IEBC kupeleka mswada wa BBI kwa kaunti kujadiliwa

Na RICHARD MUNGUTI

MCHAKATO wa ripoti ya maridhiano wa BBI umepigwa breki na mahakama kuu iliyoizima Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuendeleza harakati za kufanikisha kufanyia katiba mabadiliko.

Majaji watano George Odunga, Profesa Joel Ngugi, Jairus Ngaah, Enock Chacha Mwita na Janet Mulwa wamesitisha mchakato huo wa kufanyia katiba marekebisho hadi kesi saba zilizowasilishwa na makundi ya kutetea haki za binadamu ambazo sasa zimeunganishwa, isikilizwe na kuamuliwa.

Sasa “reggae” imesimamishwa.

Hata hivyo majaji hao wamesema ijapokuwa hawajazuia mabunge ya kaunti kujadili na kupitisha mswada uliowasilishwa na IEBC, ni sharti kuelewa “maamuzi yao yanaweza kuharamishwa kesi ya walalamishi hao saba ikiamuliwa hatimaye.”

You can share this post!

Fuata utaratibu huu kuandaa keki yenye ladha tamu

Maseneta sita wa Jubilee watimuliwa kwa ukaidi