• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
HABARI YA KIPEKEE: Maisha ya Robert Gituhu, mhandisi aliyejiteketeza kwa mafuta ya taa Mombasa

HABARI YA KIPEKEE: Maisha ya Robert Gituhu, mhandisi aliyejiteketeza kwa mafuta ya taa Mombasa

NA NYABOGA KIAGE

BW Robert Gituhu, 28, mwanamme aliyejiua katika Kaunti ya Mombasa alikuwa mwanafunzi mwerevu shuleni na hata alipata alama ya A- katika mtihani wake wa kitaifa Shule ya Upili mwaka 2012.

Bw Gituhu, mnamo Alhamisi, Agosti 17, 2023 alijitekelezea tukio hilo Jijini Mombasa kwa kujimwagilia mafuta ya taa, kisha akawasha moto kiberiti.

Kwa mujibu wa walioshuhudia, walisema alilalamikia hali ngumu ya maisha.

Kisa hicho kilishtua Wakenya wengi.

Alisoma katika Shule ya Sekondari ya Kijabe, ambapo alikuwa kiranja wa darasa na hata kupandishwa cheo na kuwa kiranja mkuu wa shule hiyo akiwa kidato cha nne.

Isitoshe, katika mtihani wake wa darasa la nane, Bw Gituhu alipata alama 400.

Akizungumza na Taifa Leo Dijitali, Bi Rose Mineh Gituhu, mamake alisema kuwa alipoteza kijana ambaye alijitolea sana kwenye masomo na hata kuhitimu katika Kozi ya Uhandisi kutoka chuo kikuu cha Eldoret.

“Alikuwa mcheshi, na mwenye kutia bidii shuleni, alikuwa mpole na pia aliheshimu kila mtu,” Bi Moneh alisimulia.

Mamake Robert Gituhu, Bi Rose Mineh Gituhu.

Hali kadhalika, alisema kuwa mwendazake alikuwa na dada mmoja tu anayejulikana kama Bi Telly Mwihaki.

Taifa Leo Dijitali ilipomuuliza shughuli ambazo mwanawe alijishughulisha nazo Mombasa, alisema; “Alitoka nyumbani siku ya Jumapili bila kusema na tulitarajia kwamba angerejea”.

Walipogundua kuwa hawakuwa wanamfikia kwa njia ya simu, waliamua kueneza ujumbe kupitia mtandao wa Facebook wakiwa na tumaini kwamba wangempata.

Msemaji wa familia hiyo, Bw Jackson Nkoidila alisema kuwa walipoteza kijana mkwasi wa bidi.

“Tulipogundua kuwa harejei nyumbani hapo ndipo tulipoamua kutangaza mtandaoni, tukiwa na matumaini kumpata. Tuliposikia kuwa kuna mtu ambaye amejitia kitanzi Mombasa, na kubaini kuwa ni yeye hatukuamini,” alisema Bw Nkoidila.

Licha ya kutokuwa na ajira, Bw Nkoidila alidokeza kwamba mwendazake akiwa hai alijikaza kisabuni kusaka kazi ila hakufaulu.

  • Tags

You can share this post!

Raila aenda kupunga unyunyu nchini Uingereza

Mwanahabari ashambuliwa na wasaidizi wa mbunge wa Maragua

T L