• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 11:39 AM
Jamhuri Dei: Ruto kuongoza taifa kuadhimisha miaka 60 ya kujitawala

Jamhuri Dei: Ruto kuongoza taifa kuadhimisha miaka 60 ya kujitawala

NA SAMMY WAWERU

RAIS William Ruto, Jumanne, Desemba 12, 2023 ataongoza nchi kuadhimisha miaka 60 ya kujitawala.

Kenya ilianza kujitawala Desemba 12, 1963 miezi sita baada ya kujizolea uhuru wa ndani kwa ndani kutoka kwa serikali ya Muingereza.

Hayati Mzee Jomo Kenyatta – Babake Rais wa Nne wa Jamhuri ya Kenya, Bw Uhuru Kenyatta, ndiye alikuwa Rais wa kwanza wa taifa hili na ambaye aliongoza Wakenya kupitia vuguvugu la MauMau na makundi mengine kuondoa Mbeberu.

Jamhuri Dei, ni Sikukuu na ya kitaifa inayoadhimishwa kila mwaka, ambayo husherehekewa Desemba 12.

Jamhuri, ni neno la Kiswahili linalomaanisha ‘Taifa’ hivyo basi Jamhuri Dei inasimamia siku maalum ambayo Kenya ilianza kujitawala mnamo Desemba 12, 1963.

Aidha, hilo liliafikika miezi sita baada ya nchi kupata uhuru wa ndani kwa ndani kujitawala – Juni 1, 1963.

Siku maalum ya uhuru wa ndani kwa ndani kujitawala huadhimishwa Juni 1, kila mwaka.

Chini ya Katiba ya sasa iliyoidhinishwa 2010 na kuanza kutumika 2013, sherehe za Jamhuri Dei pia zinaadhimishwa katika kiwango cha kaunti.

Magavana wanatarajiwa kuandaa hafla kuadhimisha miaka 60 ya Kenya kuanza kujitawala.

Aidha, kutakuwa na gwaride la heshima litakaloandaliwa na kikosi cha majeshi wa Kenya (KDF) na pia askari.

Dkt Ruto atatumia jukwaa la Jamhuri Dei 2023 kuainisha hatua ambazo Kenya imepiga mbele, kimaendeleo, miaka 60 baada ya kuanza kujitawala.

Hafla ya kitaifa inafanyika katika Bustani ya Uhuru, Nairobi.

 

 

 

 

  • Tags

You can share this post!

Wakazi walivyosaidia polisi kuua wezi, na kuokoa mbuzi 1,600

Mwanamume anayesotea jela kwa unajisi wa mtoto aokolewa na...

T L