• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 6:50 AM
Je, ni mambo gani hayana umuhimu sana maishani?

Je, ni mambo gani hayana umuhimu sana maishani?

NA MARGARET MAINA

[email protected]

MADA ya leo inaangazia mambo ambayo yamekithiri katika maisha na bado watu wengi wamenaswa nayo.

Maoni ya watu wengine

Kuishi ili kuwafurahisha wengine ni mtego unaoficha mbali kipaji chako ambao wengi wangefaidika kutokana na kipaji hicho.

Japo unaweza ukajitahidi ili kujizuia kumkosea mtu mwingine, kwa kweli, haiwezekani kumpendeza kila mtu.

Sababu hukumu ya watu wengine haina umuhimu ni kwamba watu wengi wana wasiwasi sana wakishangaa unafikiria nini juu yao.

Ipo haja ya wewe kuwa mwamuzi wa mambo muhimu yanayokuhusu hata kama itaonekana ni wewe pekee unayejijali.

Kahawa yako ya asubuhi

Ikiwa unategemea kahawa yako ya asubuhi kukupa nishati hebu fikiria vizuri; labda unapaswa kurekebisha tatizo halisi: kama vile kupata usingizi mzuri wa usiku, au kupata suluhisho katika maisha yako ambayo itakufanya uhisi kuwa mchangamfu na kuwa na nishati.

Visingizio

Bila shaka zipo changamoto maishani zinazokuzuia kupata matokeo unayohitaji maishani. Usibabaishwe na hilo. Kwa kweli, sote tunazo changamoto tofauti lakini maisha hayasimami.

Acha kuangazia kwa nini huwezi kufanya kitu, na elekeza mawazo yako katika kile unachoweza kufanya vizuri zaidi.

Visingizio havisaidii chochote maishani: havikupeleki mbele, na havichangii siku ya mtu mwingine yeyote. Badala ya kuleta visingizio, fanya kwa vitendo.

Hisia ya uimara

Wakati mwingine, unaweza kuhisi kama bado hujafikia hatua muhimu za maisha.

Wengi wetu tunataka kushikamana na hisia ya uimara na kufanya mambo kwa njia fulani ili kudumisha wazo la uhakika. Suala na hilo, ni kwamba kila kitu kiko na usawa na kubadilika kila wakati: kama vile mwili wako unavyobadilika, ndivyo pia ulimwengu unaokuzunguka unavyobadilika.

Uimara haupo kabisa: Mabadiliko ni mara kwa mara, na ni wakati tu unapojifunza kukabiliana na kusonga nayo, kwamba unaweza kupata hisia yoyote ya utulivu. Kusonga kwa kasi ya maisha ndiyo njia pekee ya kuwa sehemu ya mabadiliko, na sio mwathirika wake.

Hasira/chuki

Hufai kabisa kuweka kinyongo dhidi ya mtu au jambo lililokupata. Kwa kweli, unajua kwamba hukumu ya watu wengine sio muhimu, hasa ikilinganishwa na yako mwenyewe.

Kinyongo kinakuzuia kusonga mbele. Kinakufanya tu kukwama katika siku za awali. Kwa kweli hakuna anayejali, na wewe pia unapaswa kutojali.

Badala yake, tafuta njia mpya za kusonga mbele. Tafuta mambo unayoweza kufanya vyema wakati ujao, kwa sababu wewe ndiye unayeweza kudhibiti mawazo na maisha yako.

  • Tags

You can share this post!

Gharama ya maisha kupanda zaidi kufuatia kuongezeka kwa bei...

Raila asijaribu kuzua vurugu wakati wa maandamano, Ruto...

T L