• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 5:17 PM
JIJUE DADA: Je, huwa unahisi uchungu unaposhiriki tendo la ndoa?

JIJUE DADA: Je, huwa unahisi uchungu unaposhiriki tendo la ndoa?

NA PAULINE ONGAJI

UCHUNGU wakati wa tendo la ndoa (dyspareunia) hutokea sana katika sehemu ya ndani ya uke.

Utafiti uliofanywa hivi majuzi ulionyesha kuwa zaidi ya asilimia 60 ya wanawake, hukumbwa na hali hii.

Visa hivi vinasemekana kuongezeka kutokana na sababu zifuatazo:

• Mabadiliko ya mbinu zinazotumika wakati wa ngono.

• Kuongezeka kwa magonjwa ya zinaa.

• Uhuru na uwazi wa kujadili masuala haya siku hizi.

Uchungu unaoshuhudiwa wakati wa kushiriki tendo la ndoa huchunguzwa na daktari wa kawaida au mwanajinakolojia.

Wataalamu wengine wanaoweza kuhusishwa ni pamoja na daktari wa akili, mwanasaikolojia au mtaalamu wa mfumo wa viungo vya uzazi na mkojo kama vile figo na kibofu.

Ingawa wakati mwingi uchungu huu haupaswi kuzua wasiwasi, unashauriwa kutafuta usaidizi wa kimatibabu kila unaposhuhudia ishara zifuatazo:

•Uchungu mwingi unaosababisha damu kuvuja kutoka sehemu ya uke.

• Kichefuchefu, kutapika au uchungu katika sehemu ya rektamu hasa baada ya kushiriki ngono.

•Kutokwa na majimaji yasiyo ya kawaida baada ya kushiriki ngono.

Chanzo

• Kutolainisha vyema sehemu ya uke kabla ya kushiriki tendo la ndoa, hali ambayo hutokana na mabadiliko ya kihomoni au matumizi ya dawa fulani.

• Kuvimba katika lango la uke.

• Mkazo au mshtuko wa ghafla katika sehemu ya ndani ya uke.

•Uchungu katika sehemu yote ya uke unaashiria kuharibika kwa misuli ya sehemu hii, hali nyingine isiyo ya kawaida au maambukizi ukeni.

•Uchungu unaotokea wakati wa kushiriki ngono ambapo mwanamume atahisi kana kwamba amejigonga kwa kitu, unashiria chupa ya uzazi iko katika sehemu mbaya au kulegea kwa mayai ya uzazi.

Mbinu rahisi ya kukabiliana na shida hii ni kupaka mafuta maalum yanayotumika kulainisha sehemu ya ndani ya uke wakati wa kushiriki tendo la ndoa.

You can share this post!

Kiungo Starlets arejea nchini baada ya majaribio Austria...

Tungali imara, maseneta wa Azimio wasema

T L