• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
Jinsi ya kuandaa milkshake ya biskuti

Jinsi ya kuandaa milkshake ya biskuti

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 5

Wanywaji: 2

Vinavyohitajika

Maziwa 500ml (nusu lita)

Biskuti pakiti 3 za Nuvita (unaweza ukatumia biscuits aina nyingine yoyote)

Sukari kiasi

Iliki iliyosagwa kijiko 1 kidogo

Vanilla/ice cream flavour (sio lazima)

Maelekezo

Chemsha maziwa na iliki kisha acha ili kuhakikisha vyote hivi vinapoa.

Weka biskuti kwenye maziwa kwa dakika moja.

Weka mahitaji yote kwenye blenda na upige kwa sekunde 30 (nusu dakika).

Shake iko tayari. Iweke kwenye jokovu.

Mimina kwenye glasi ufurahie kwa keki au kitafunio chochote upendacho.

You can share this post!

Shughuli ya kuhesabu kura Juja yaendelea baada ya vurugu...

Umuhimu wa divai nyekundu kwenye ngozi na nywele