• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 3:42 PM
Kesi dhidi ya Ruto kuhusu unyakuzi wa nyumba kuendelea

Kesi dhidi ya Ruto kuhusu unyakuzi wa nyumba kuendelea

Na JOSEPH WANGUI

MAHAKAMA kuu imeagiza kesi ya unyakuzi wa jumba la kifahari aliyoshtakiwa Naibu wa Rais, Dkt William Ruto miaka 13 iliyopita na Tume ya Kukabiliana na ufisadi (EACC) ianze kusikizwa hadi tamati.

Jaji Samuel Kibunja aliyetoa agizo hilo pia alikubali ombi la EACC kuwashtaki washukiwa wengine 17 pamoja na Dkt Ruto.Jaji Kibunja alitupilia mbali ombi la kampuni ya Magut Agencies inayohusishwa na aliyekuwa Meya wa Mji wa Eldoret, Bw Josiah Kiprotich Magut.

Katika ombi lake, Magut Agencies iliomba mahakama ikubaliane na uamuzi wa Tume ya Taifa ya Ardhi (NLC) kuhusu umiliki wa jumba hilo pamoja na ardhi ilikojengwa.Kesi dhidi ya Dkt Ruto iliwasilishwa hapo awali na iliyokuwa tume ya kitaifa ya kukabiliana na ufisadi (KACC), kuhusu umiliki wa jumba hilo lililoko mtaa wa Elgon View mjini Eldoret.

KACC ambayo sasa ni EACC iliomba mahakama, Serikali ikubaliwe kutwaa jumba hilo ikidai limejengwa katika ardhi ya umma.KACC ilisema Dkt Ruto alinyakua jumba hilo mnamo 2005 alipokuwa Mbunge wa Eldoret Kaskazini.

Ardhi ambamo jumba hilo limejengwa ilikuwa imetengwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa ngazi za juu katika Baraza la mji wa Eldoret. Mbali na Magut Agencies, wengine walioshtakiwa ni aliyekuwa Kamishna wa Ardhi Wilson Gachanja na kampuni ya Somog Ltd.

Ardhi ambayo jumba hilo linalomilikiwa ni Dkt Ruto inapatikana ina hatimiliki namba: Eldoret Municipality Block 8/574, na ilitengwa kutoka kwa hatimiliki asili nambari Block 8/83.Ardhi hii ilikuwa imepewa Magut Agencies na Bw Gachanja.

Baadaye shamba hilo lilisajiliwa kwa jina la Dkt Ruto. Hati za umiliki wa shamba hilo zilifutiliwa mbali mnamo 2010 na aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Bw James Orengo, ambaye sasa ni Seneta wa Siaya.

Ushahidi wa KACC ambayo sasa ni EACC unasema ardhi hiyo ilinyakuliwa.

You can share this post!

Maafisa tisa Kuppet wamezea mate siasa

EACC yaambia Waiguru ‘tuliza boli’

T L