• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:55 AM
KIDIJITALI: Apu ya ‘Kalro Garlic’ kusaidia wakulima wanaoazimia kukuza vitunguu saumu nchini

KIDIJITALI: Apu ya ‘Kalro Garlic’ kusaidia wakulima wanaoazimia kukuza vitunguu saumu nchini

NA LEONARD ONYANGO

JE, wajua kuwa asilimia 50 ya vitungu saumu vinavyotumiwa humu nchini vinaagizwa kutoka ng’ambo, haswa nchini China?

Takwimu za serikali zinaonyesha kuwa Kenya huzalisha tani 2,000 za vitunguu saumu kila mwaka.

Kenya inahitaji angalau tani 4,000 kila mwaka ili kutosheleza mahitaji ya bidhaa hiyo nchini.Vitunguu saumu ni miongoni mwa mazao yanayoleta hela nyingi katika kipande kidogo cha shamba.

Inakadiriwa kuwa robo ya ekari ya vitunguu saumu inaweza kuleta Sh300,000.

Vitunguu saumu hufanya vyema katika sehemu nyingi za nchini, haswa maeneo yaliyo na maji ya kutosha.Nchini Kenya, vitunguu saumu hukuzwa kwa wingi katika Kaunti za Narok, Nakuru na Meru.

Lakini wataalamu wanasema kuwa zao hilo linaweza kufanya vyema hata katika maeneo ya Magharibi mwa Kenya.Apu ya simu inayofahamika kama ‘Kalro Garlic’ inaweza kusaidia pakubwa wakulima wanaotaka kuanzisha kilimo cha vitunguu saumu kupata maarifa.

Apu hiyo inaweza kupakuliwa kutoka katika mtandao wa ‘Play Store’.Kulingana na ‘Kalro Garlic’, mkulima anayetaka kuanzisha kilimo cha vitunguu saumu ni sharti aepuke shamba ambalo limekuwa likikuzwa vitunguu vya kawaida kwa miaka mitatu mfululizo.

Apu hiyo inakupa maarifa kuhusu namna ya kuandaa shamba, jinsi ya kupata mbegu zifaazo, mbolea inayohitajika na kuhifadhi mavuno.

Kwa mfano, apu hiyo inashauri kuwa unapopanda vitunguu saumu ni sharti uvitenganishe umbali wa inchi 6 ili kufanya vyema.

  • Tags

You can share this post!

West Ham wasajili kipa matata wa PSG, Alphonse Areola, kwa...

Maajenti wa kazi Uarabuni kuchunguzwa

T L